Mapema mwaka jana, mwandishi wa VOA alipokea simu kutoka kwa chanzo cha uhakika kikimueleza kutarajia mzigo muhimu. Siku chache baadaye, mzigo ulifikishwa katika boksi dogo la kahawia. Ndani, kwa makini zilifungwa kwa karatasi kadhaa za plastiki, kulikuwa na hard drive ndogo. Ilikuwa na zaidi ya mafaili 400 ya video — kitu ambacho kiligeuka na kuwa ni saa 18 za rekodi.
Ukiangalia video chache, mwandishi ameshangazwa: Watu katika video walikuwa wapiganaji wa Boko Haram, moja ya makundi mabaya sana na yenye usiri mkubwa duniani. Wanachama karibu wengi hawajahi kuonyesha nyuso zao hadharani, lakini katika rekodi hizi za video ambazo zimechukuliwa na mpiga video, wanamgambo wanaonekana wazi wazi wakizungumz, wakijigamba na kuendelea na shughuli zao za kila siku — na bila ya khofu wakitenda mauaji mbaya.
Kanda za video zinaonyesha wazi wazi kwanini zaidi ya wanigeria milioni mbili wamekimbia kwenye miji na vijiji vyao kuepuka ghadhabu za Boko Haram. Miongoni mwa mambo mengine, video zinawaonyesha Boko Haram wakiwauwa na kuwapiga bakora raia, kuwakata mikono watu, kushambulia vituo vya jeshi na kuwauawatu katika msako wa kutafuta fedha na chakula. Wanamgambo wanaonyeshwa wakiwahoji wana vijiji, wakirusha ndege zisizo na rubani na wakiwalaani kwa ukali “wasioamini” wakiwashutumu kwa kukiuka misingi ya uislamu ambao wameipotosha.
VOA imebaini kuwa kanda hizo za video zimetoka kwenye laptop ya Boko Haram ambayo ilikamatwa katika uvamizi uliofanywa na jeshi la Nigeria. Chanzo cha video hizo hana uhusiano na jeshi la Nigeria wala serikali, au na Boko Haram.
Waandishi wa VOA wlianza kuchambua video hizo. Waliwahi kuona propaganda za Boko Haram katika video hapo kabla, lakini hili lilikuwa la kipekee: rekodi ambazo hazikuhaririwa zimefanya mabadiliko kidogo au hakuna juhudi iliyofanywa kuficha vitendo vya kinyama vya kundi hilo. Kwaishara zote – muda wa video zilipochukuliwa, utambulisho wa wapiganaji, matukio yaliyoelezewa katika matangazo ya habari zinasikika kwa mbali — rekodi hizo zilichukuliwa mwishoni mwa 2014 na 2015, kipindi cha upanuzi uliofanywa na Boko Haram kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Wafanyakazi wa VOA walitumia miezi kadhaa kutathmini hizo video, kuondoa mashaka yoyote kuhusu uhalali wa kwa kutafsiri yaliyomo ndani na kulinganisha na maeneo kwa kutumia picha za satalaiti. Wapiganaji wakiongea kwenye kamera walijitambulisha wenyewe kwa Boko Haram na wengi wanazungumza lugha ya Kanuri, lugha inayotumiwa na kundi hilo. Bendera za Boko Haram na nembo mara kwa mara vinaonekana wazi wazi. Walau kipande kimoja cha video kilitumiwa katika video za propaganda za Boko Haram ambazo zilitolewa hadharani. VOA pia ilisafiri kwenda Nigeria Septemba mwaka 2016 kutembelea maeneo yaliyoonyeshwa kwenye video, wanigeria waliokoseshwa makazi walisaidia kuyatambua maeneo ambako mauaji yalirekodiwa.
VOA imeonyesha baadhi ya vipande vya video kwa Jacob Zenn, msomi katika Jamestown Foundation, shirika lenye makao yake Washington DC., ambaye alisomea kwa kina kuhusu Boko Haram. Zenn aliweza kuwatambua baadhi ya wanamgambo wa Boko Haram waliokuwemo katika video. Amesema rekodi hizo zimetoa mtizamo bayana kuhusu kazi za ndani za kundi hilo.
Tangu kanda za Boko Haram zirekodiwe, na katika miezi tangu VOA ilipozipata, jeshi la Nigeria limepata mafanikio makubwa katika kuichukua tena miji na eneo ambalo liliwahi kushikiliwa na Boko Haram. Maafisa wa jeshi na rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari anasema kundi limelazimishwa kutoka kwenye mojaya maficho yake makuu katika msitu Sambia. bado, Boko Haram linaendelea kufanya mashambulizi kwenye malengo ya kijeshi na kiraia.
Mwezi Januari, VOA ilimuonyesha baadhi ya picha kutoka kwenye video Waziri wa Ulinzi wa Nigeria, Mansur Mohammed Dan Ali, ambaye amesema hajawahi kuziona hapo kabla na hakufahamu kama kulikuwa na video kama kama hizo. Lakini alipoangalia matukio ya wanamgambo wa Boko Haram wakiwapiga bakora na kuwaua wana vijiji, waziri alijizuia sana kulia.
Dan Ali amesema kwamba wakati utawala wa Buhari ukiwa umepata maendeleo dhidi ya Boko Haram, video zilizorekodiwa zinaikumbusha dunia kuwa kundi hilo hali majuto hata kidogo kwa ukatili wao.
JIFUNZE ZAIDI
Angalia ripoti mbali mbali za mitandao ya habari.
Angalia mfululizo wa “Boko Haram: Ugaidi Wafichuliwa”.
Soma kuhusu mapigano ya Nigeria dhidi ya Boko Haram.
WATU WANASEMAJE
Hirikiana mawazo yako kuhusu "Boko Haram: Ugaidi Wafichuliwa" #terrorunmasked..
Facebook
Twitter