Kumsikia Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari akisema, Boko Haram limekwisha. Siku moja kabla ya Krismas, alitangaza kwamba wanajeshi wamekamata maficho ya mwisho ya wanamgambo katika msitu mkubwa wa Sambisa. Amesema ukamataji huo umeadhimisha “ kulivunja kabisa Boko Haram,” na kwamba kwa mujibu wa mkuu wake wa jeshi, “magaidi wanakimbia na kamwe hawana sehemu ya kujificha.”
Siku mbili baadaye, walipuaji mabomu wa kujitoa mhanga – wote wanawake – walilenga soko la ng’ombe huko Maiduguri, wenye wakazi milioni 1.1 ni mji mkubwa uliopo kaskazini mashariki mwa Nigeria. Mlipuaji mmoja wa bomu alijiua mwenyewe, wakati mwingine alipigwa na kundi la watu kabla ya kutegua milipuko yake. Hakuna aliyedai kuhusika lakini tuhuma zilielekezwa kwa Boko Haram, ambalo walipuaji wake wa kujitoa mhanga, wengi wao wanawake, wameua maelfu ya wanigeria kwenye maeneo ya umma katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Wanigeria wachache walishangazwa na shambulizi hilo. Buhari na kiongozi aliyemtangulia Goodluck Jonathan waliahidi ushindi juu ya Boko Haram katika siku zilizopita, ghafla tu wimbi jipya likaonekana la ghasia za mauaji upande wa kaskazini mashariki. Kama vita dhidi ya kundi la kiislamu lenye msimamo mkali vinapata maendeleoe – na kwa vigezo vya baadhi, ndiyo – maendeleo hayajamaliza madhila yanayowakabili mamilioni ya wanigeria wanaojaribu kukabiliana na uharibifu wa nyumba zao, kupoteza hali ya maisha yao, ugavi usioeleweka wa chakula na maji, wasi wasi kuhusu kutekwa nyara kwa marafiki na wanafamilia, na pia kuna uwezekano mkuubwa kwamba mlipuaji bomu wa kujitoa mhanga wa Boko Haram ataonekana kwenye soko la eneo au kituo cha basi.
Inapokuja vitisho vya kigaidi, Islamic State na al-Qaida mara nyingi ndiyo hufikiriwa kuwa ndiyo makundi yenye sifa mbaya sana. Lakini mwaka 2014, Boko Haram liliua watu wengi zaidi kuliko kundi jingine lolote lenye msimamo mkali duniani, na mwaka 2015 lilikuwa la pili nyuma ya IS. Hivi sasa, VOA News imepata kanda kadhaa za video ambazo zilirekodiwa na Boko Haram zinazobaini utendaji kazi wa ndani kwa undani wa kikatili, na kusisitiza kwanini bado ni moja ya kundi la kijihadi ambalo linakhofiwa sana kila mahali.
Katika moja ya matukio mengi ya kutisha sana, ambalo huenda lilirekodiwa mwishoni mwa 2014, wanamgambo katika kijiji cha Kumshe waliwalazimisha wakazi kuangalia kuchapwa viboko kwa watuhumiwa 10 waliodaiwa kutumia madawa na wengine kuambiwa wawapige bakora. Halafu, wakati wanavijiji walipokuwa wakisema “Allahu Akbar,” wanaume watatu walioshutumiwa kwa kuuza dawa walipigwa risasi kwenye moyo na kichwa na kuuwawa.
Mauaji yanapofanyika, mmoja wa wawauaji anatangaza: “Sisi tumetimiza amri ya mwenyenzi mungu,” wakati miili na wanaume waliokufa iliyojaa damu ikiwa imelala nyuma yake.
Tukio hili na mengine yanawaonyesha wanachama wa Boko Haram wakishuhudiwa wakiendelea na maisha yao ya kila sikukatika eneo ambalo wamejitangazia ukhalifa hii imo katika mfululizo wa sehemu nne za video za VOA, “Boko Haram: Ugaidi Wafichuliwa.” Video hizi ambazo zilirekodiwa awali zinaonyesha hali ya kutisha sana ya kila ambacho kinaikabili Nigeria wakati ambapo serikali inadai kwamba imepata maendeleo katika vita ambavyo vimechukua maisha ya takriban watu 18,000 na kushuhudia kutekwa nyaraka kwa maelfu ya wanawake na watoto kulikofanywa na Boko Haram.
Mafanikio yoyote ya karibuni ambayo jeshi imeyapata, safari ya kuelekea kupona bado ni ndefu.
Jacob Zenn, mtalaamu wa masuala ya Afrika katika taasisi ya Jameston, inayofuatilia masuala mbali mbali yenye makao yake Washington, D.C., amesema ushindi wa kweli wa jeshi kwa Boko Haram uko walau umbali wa miaka mitatu au mitano ijayo. Wakati huo, amesema, inawezekana kundi hilo, “likaweza kusukumwa mbali zaidi na kaskazini mashariki mwa Nigeria na kupunguzwa kuwa kitu cha hatari, na siyo tishio kwa uhuru wa Nigeria kama lilivyokuwa.”
Lakini huo ni mwanzo tu. Kujenga tena shule za mkoa peke yake kutachukua miaka kadhaa. Nyingi zimechomwa na Boko Haram, ambalo jina lake lina maana kwa lugha ya Kihausi kuwa “ Elimu ya magharibi ni haramu.” Umoja wa Mataifa, katika ripoti yake ya karibuni kuhusu mahitaji ya kibinadamu kaskazini mashariki mwa Nigeria, imesema watoto milioni 3 walio katika umri wa kwenda shule hawana fursa ya kupata elimu. Na inakadiriwa kuwa wanigeria milioni 1.7 bado wamekoseshwa makazi kutokana uharibifu kwenye nyumba na vijiji.
Baadhi ya ujenzi umeanza. Bado, wakijaribu kuleta uthabiti kaskazini mashariki, sehemu kubwa na eneo la ndani zenye miji iliyotawanyika na vijiji ambako waasi wa Boko Haram wanaendelea kufanya shughuli zao, huenda ikachukua miongo kadhaa, Zenn amesema.
“Hili mara nyingine linawashangaza wanigeria ninaposema hivi, lakini nadhani itachukua walau miaka 20,” amesema.
“Itachukua kizazi kzima kujenga jamii kurejea tena katika maisha ya kawaida baada ya mzozo ambao umewakumba watu katika nchi hiyo.”
Mji Mmoja, Umeharibiwa Mara Nne
Lengo la Boko Haram, akama ilivyoelezwa na kiongozi wa muda mrefu Abubakar Shekau katika video za propaganda, ni kuitisha vita vya kidini, kuuondoa uislamu na Nigeria katika ushawishi wa Magharibi na kuunda ukalifu ambako sheria kali za kiislamu ndiyo zitakazotawala. Lakini kimsingi, kundi hilo limeonyesha huruma ndogo sana kwa waislamu wanigeria, kushambulia baadhi ya misikiti na miji yenye waislamu wengi.
Take Mainok, mji mdogo kiasi cha kilometa 60 magharibi mwa Maiduguri. Mara nne tangu Machi 2014, majeshi ya Boko Haram yaliingia mjini humo, yameua dazeni ya watu kila wakati na kuziharibu kabisa nyumba, maduka, mashule, kituo cha afya na kituo cha polisi.
VOA News iliitembelea Mainok mwezi Septemba mwaka 2016 katika safari ya kuripoti yaliyoonyeshwa kwenye video za Boko Haram. Chifu wa kieneo Lawan Bukar Kyari ameiambia VOA kwamba wakazi hawakuwa na njia ya kujitetea wenyewe. “Wakati Boko Haram walipotushambulia kushoto na kulia, hatukuwa na usalama wowote hapa. Tulikuwa tu na kituo chenye polisi wanne,” amesemma. “Wanafika hapa wanavyotaka, na wanuuwa watu na wanaondoka bila ya mtu yoyote kukabiliana nao. Tulitaabika sana kwa miaka miwili au mitatu na kila aliondoka humu mjini…Boko Haram waliuwa zaidi ya watu 200 mjini humu.”
Tangu serikali ichukua tena mji mapema mwaka jana na kuweka kituo cha jeshi, watu wameanza kurejea pole pole, na Mainko inajengwa tena kwa mara ya nne. “Watoto wetu hawajakwenda shule kwa miaka mitatu iliyopita, “ amesema Kyari.
Bahati mbaya, hadithi ya Mainok si ya kipekee. Sehemu katika jimbo la Borno, kiini cha uasi, kimsingi huwezi kuishi. Gavana Kashim Shettima ameiambia VOA kwamba kwa mujibu wa utafiti wa karibuni wa Benki ya Dunia, Boko Haram limeharibu zaidi ya nyumba 950,000 kote katika jimbo hilo, kiasi cha asilimia 30 ya akiba ya nyumba. Wanamgambo pia wameharibu zaidiya madarasa 5,000, kiasi cha vituo vya afya 200 na zaidi ya vyanzo 1,000 vya maji, amesema, na kudumuaza uwezo wa uzalihsaji umeme.
“Inatisha sana, kiwango cha uharibifu,” Shettima amesema.
Pengine hakuna mtu aliyathirika zaidi kuliko wakazi wa Bama, kituo cha biashara kilichopo kusini mashariki mwa Maiduguri, karibu na mpaka na Cameroon. Wapiganaji wa Boko Haram waliukamata mji huo wenye takriban wakazi 300,000 mwezi Septemba 2014 na kuugeuza mji usiokuwa na watu. Mamia ya wakazi walichinjwa na wanamgambo kabla ya wengi wengine kukimbia. Video ya kutisha ambavyo imeibuka kwenye mtandao imewaonyesha watu waliokuwa na silaha wakiwaburuza watu kwenye daraja lililo juu yam to Yedzaram, kuwapiga risasi kichwani, na halafu kuwatupa ndani ya maji.
Miundo mbinu Bama haikusalimika. Shettima amesema kiasi cha asilimia 90 ya mji uliharibiwa; waandishi wa VOA ambao walikwenda huko kuthibitisha kwa macho yao, waligundua mtaa baada ya mtaa ukiwa hauna watu na kuna majengo yaliyochomwa moto.
Gavana aliahidi kwamba miji katika jimbo iliyoharibiwa itajengwa tena, kwa kutumia vifaa vya ndani na nguvu kazi ya ndani kupunguza ukosefu wa ajira. “Tunajenga nyumba, mashule, kliniki, ili kutoa changamoto kwa maneno ya Boko Haram, pia tunajenga misikiti,” amesema.
Lakini mahitaji ya haraka ni makubwa mno. Shirika la Kimataifa la Uhamiaji limeripoti mwezi Januari kwamba robo ya takriban wanigeria milioni 1.7 waliokoseshwa makazi na uasi wa Boko Haram wanaishi katika kambi au maeneo yanayofanana na kambi.
Sehemu za Borno ambako wafanyakazi wa misaada hawawezi kufika kwa usalama huenda wakataabika kutokana na njaa, kwa mujibu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu OCHA, na kiasi cha wanigeria milioni 5 wanakabiliwa na “uhaba mkubwa wa chakula na virutubisho” Kwa kiwango kidogo, hali ni sawa katika sehemu za nchi jirani za Chad, Niger na Cameroon, ambako Boko Haram ina kambi zake na kufanya mashambulizi tangu mwaka 2013.
Hali ya chakula huenda isiboreke haraka, OCHA imeonya, wakati “mzozo na hatari ya vifaa vya milipuko vinaweza kudumaza juhudi za kilimo kwa mwaka wa tatu mfululizo.” Shettima amepongeza juhudi za UNICEF, shirla la Mpango wa Chakula duniani na bilionea raia wa Nigeria, Aliko Dangote kwa kuwasaidia watu kujaribu kurejea tena katika hali ya kawaida. Na wakati ambapo hayawezi kuwa mabaya zaidi kuliko yaliyovyo kwa njia yoyote ile, bado ana imani mambo mazuri yako mbele.
“Kimsingi tuko kwenye eneo la sifuri. Siongezi chumvi,” ameiambia VOA News. “ Watu wetu hata katika nyakati nzuri ni maskini wa maskini. Boko Haram imewatia katika ufukara mkubwa. Lakini si kwetu sisi kuanza kulalama kuhusu hatima yetu, lakini tunachukua hatua madhubuti kuelekea katika kujiweka sawa katika maisha yetu.”
Hilo likiwa limesemwa, hakutakuwa na hatua za kusonga mbele mpaka serikali ya Nigeria, ifanye kazi na majriani zake, kuweza kuhakikisha kwamba Boko Haram halirejei tena.
‘Mmetuuwa Mara Ngapi?’
Kwa sehemu kubwa ya 2014, Boko Haram lilionekana kufanya vitendo bila ya khofu. Mwezi April, kundi hilo liliwateka wasichana 276 kutoka shule moja mjini Chibok; wengi wao hadi hivi leo hawajulikani walipo. Mwaka ulivyokuwa unasonga mbele, wanamgambo walikamata udhibiti wa miji kadhaa katika majimbo ya Borno, Yobe na Adamawa. Mwezi August mwaka huo, kiongozi Shekau alitangaza kuundwa kwa ukhalifa, utawala ukiwa chini ya tafsiri kali ya sheria ya kiislamu.
Halafu kundi hilo lilienda mbali zaidi. Hapo Januari 24, 2015, mamia ya wanamgambo walijaribu kuivamia Maiduguri, mji mkuu wa jimbo la Borno, kutoka pande mbili. Wanajeshi waliwasukuma nyuma kwa msaada wa mashambulizi ya anga ya jeshila Nigeria. Wiki moja baadaye, wapiganaji wa Boko Haram waliishambulia tena Maiduguri, mara hii kutoka upande wa tatu. Kwa mara nyingine jeshi liliwasukuma kando, kwa msaada wa jeshi la anga na wapiganaji kutoka taasisi ya wanamgambo, Civilian Joint Task Force, baadhi yao ambao waliingia katika mapambano ya silaha wakiwa na mapanga na marungu tu.
Boko Haram: Raia Wameuwawa
Kushindwa kwa mashambulizi kulivunja kasi ya Boko Haram, na katika muda wa wiki kadhaa jeshi, likisaidia na majeshi kutoka Chad na Cameroon, walianza kuwasukuma magaidi kutoka kwenye maeneo yenye raia. Lakini mambo yalibadilika mwishoni mwa utawala wa rais wa zamani Goodluck Jonathan, ambaye aliondolewa mamlakani katika uchaguzi wa Mach na Muhammadu Buhari, mtawala wa zamani wa kijeshi ambaye aliijenga kampeni yake ya urais kwa kiasi kikubwa kwa ahadi ya kumaliza uasi.
Tangu Buhari achukue madaraka, operesheni za pamoja za kijeshi zinazohusisha Nigeria na majirani zake zimepata maendeleo yasiyopingika. Boko Haram kamwe halidhibiti tena miji yoyote mikubwa nchini Nigeria, na ulipuaji mabomu wa kujitoa mhanga na mashambulizi kwa malengo ya kijeshi yamekuwa ni machache na ya mauaji kuliko ya miaka iliyopita.
“hali ya sasa, naweza kusema, kwa hakika ni ya utulivu,” waziri wa ulinzi wa Nigeria, Mansur Mohammed dan Ali ameimbia VOA mapema mwezi Januari. Wanajeshi wanaona mashambulizi mashache ya kuvizia amesema.
Lakini utulivu, kwa kiwango Fulani upo, siyo sawa na amani. Wapiganaji wa Boko Haram bado wanakwenda kwenye malengo na mara nyingine wanafika huko. Mwezi Novemba 2016, kundi hilo liliua maafisa wawili wa Nigeria katika uvamizi wa kuvizia katika jimbo la Borno, ikiwemo mmoja ambaye ni kamanda wa jeshi, Luteni Kanali Muhammad Abu Ali. Mwanzoni mwa Desemba, mashambulizi pacha ya mabomu katika mji wa Madagali yameua zaidi ya watu 230 walfiariki katika shambulizi la anga, ambalo jeshi la anga liliita ni ajali na kuahidi kufanya uchunguzi.
Hivi karibuni, jeshi limelenga katika kuwang’oa Boko Haram kutoka katika kambi nyingi ndogo ndogo. zilizoko katika msitu Sambisa na maeneo ya milimani, mapango na maeneo ya ndani ya vijijini huko Borno. Jinsi Brigadia Jenerali Victor Ezugwu alivyoelezea, wanajeshi wamejihusisha katika mchezo wa paka na panya na wanamgambo.
“Kitu gani kinatokea tunapoharibu kambi hizi, mabako ya Boko Harak yanajaribu kujikusanya tena na kuweka kambi mpya,” amesema. “Kambi zilipoharibiwa miezi miwili iliyopita, tunakwenda tena na kama kuna harakati katika kambi, tunaziharibu tena. Kambi hizi hazigharimu fedha nyingi kuziweka tena. Wanaangalia sehemu chini ya miti, wanaangalia sehemu katika vilima, ambako wanaweza kujificha. Pengine hata hawaweki kitu chochote hapo. Wanaishi kama wanyama.”
Jambo jingine Boko Haram ambao wanaendelea kurejea ni kwa njia isiyo ya kawaida, kiongozi ameelezea kwa ghadhabu. Walau mara tatu, jeshi la Nigeria lilitangaza Abubakar Shekau amefariki – mara anaonekana amejitokeza katika kanda mpya za video, akitosha vitisho kwa mtindo wake kuonyesha ufyatuaji risasi, kurusha mkono wake hewani, kucheka kwa kejeli na mara nyingine akiiga kama kama ndege. Kulingana na vituko vyake katika video, Shekau anaweza kuwa muigizaji wa vichekesho, kama matamshi yake hayakuwa ya mauaji mabaya.
Kuonekana kwake karibuni ilikuwa mwishoni mwa Desemba katika video ambayo aliyapuuza madaki ya Buhari kwamba Boko Haram limetokomezwa kutoka msitu Sambisa. “Uswaambie watu uongo,” amesema kwa lugha ya kihausa. “Kama umetokomeza sisi, mnaweza kuniona mimi kama hivi? Mara ngapi mmetuuwa katika mauaji yenu ya uongo?”
‘Kama Hatusitishi Chuki Hizi….’
Ukweli ni kwamba Boko Haram haliwezi kutokomezwa, siyo moja kwa moja. Mpaka jamii ya wanaigeria izungumzie matatizo ambayo yamechochea kuundwa kwake. Nigeria ni mzalishaji mkubwa wa mafuta barani Afrika na utajiri wa nchi hiyo katika misingi ya pato la jumla la ndani, lakini mafuta yako upande wa kusini na mapato yanapatikana kwa kiasi kikubwa yamebaki na wasomi. Wachambuzi wachache wanahusisha kupanda kwa Boko Haram na umaskini sugu uliopo kaskazini mashariki mwa Nigeria, na serikali imeshindwa kupunguza hilo.
Maafisa wa Ngieria hawana “nguvu mubwa” ya kuwasaidia watukatika eneo hilo amesema Zenn, ambaye kwa kiasi kikubwa amefuatilia masuala ya Boko Haram. “Hivi ni vijiji vya ndani mno, kwahiyo siyo kwamba watu wana utiifu kwa serikali kulingana na muingiliano wake wa huduma.”
Kuna masuala ya ekolojia, ameongezea. “Kuna watu ambao wanapoteza hali yyao ya masiha kutokana na eneo kugeuka jangwa, na bila ya ajira Boko Haram ni aina Fulani ya ajira kwaa.”
Kama ilivyo kwa makundi mengine kote Afrika na Mashariki ya kati, Boko Haram pia linachukua theolojia ya kiislamu na kuibadili ili kuhubiri ghasia, ambayo inaweza kuwavutia vijana ambao wanaona hakuna cha kufanya isipokuwa kupambana katika maisha yao. Video za Boko Haram ambazo VOA imezipata zinawaonyesha viongozi wakitoa mafunzo ambayo yanaondoka kabisa katika uislamu wa kweli.
Video moja ilimuonyesha kamanda akitoa mafundisho kwa wapiganaji wake kabla ya shambulizi: “mwenyenzi mungu amesema lazima tupambane na wale ambao hawaamini dini yetu,” amesema: “ Kwa uislamu kuenezwa lazima kuwepo na umwagaji damu – ama sisi au wale wasioamini.”
Na katika video nyingine, mjumbe wa Shekau aliuambia umati, “mwenyenzi mungu ametujaribu kwa kutuletea ndumila kuwili miongoni mwetu. Katika dini yoyote ambayo mtaishi kwa amani na wasioamini haitoki kwa mitume.”
Wasomi wa kiislamu wa Ngieria ambao walizungumza na VOA walipinga kabisa tafsiri hii.
“Kuna tatizo katika uwelewa wao wa uislamu,” amesema profesa Ibrahim Mohammed, mkurugenzi wa Kituo cha Masomo ya Koran katika chuo kikuu cha Bayero huko Kano. “Kuna upotoshaji na kutafsiri vibaya katika kusoma aya za koruan nje ya mazingira yake.”
“Unaposoma aya hizi tatu pamoja, zitakupa sifuri,” amesema.
Khalifa Aliyu Abul Fathi, kiongozi wa wasomi wa kisufi wa kiislamu huko Maiduguri, alikubaliana na hilo.
“Wamefuata misingi gani ya kiislamu? Hakuna. Wameuwa wanawake. Wameuwa watoto. Wameuwa raia wasiokuwa na hatia. Na wameuwa wakristo ndani ya makanisa katika nyumba zao,” amesema.
Fathi alibashiri kwamba makundi yenye itikadi kali kama Boko Haram yataendelea mpaka uislamu utatue mjadala wa migogoro ya ndani. ‘kama hatuwaondoi chuki miongoni mwetu, tutakuwa tumemalizana na Boko Haram lakini tutakuwa tunakabiliana na kundi jingine lenye jina tofauti,” amesema.
“Wengi walioko huko nje wanaunda makundi kwasababu ya imani. Imani inahitaji kushughulikiwa.”
Mvunjiko Ndani ya Boko Haram
“Kundi jingine” huend atayari limeibuka nchini Nigeria. Mwanzoni mwa 2015, Shekau aliahidi ushirika na kundi la wanamgambo wa Islamic State lenye makao yake nchini Iraq. Lakini mwezi Agosti mwaka jana, IS lilimpa Shekau mgongo, na kumtaja Abu Musab al-barnawi – mtoto wa kiume wa marehemu muanzilishi wa Boko Haram – kuwa kiongozi mpya wa kundi hilo.
Shekau aliyeghadhibika aliipinga hatua hiyo katika ujumbe wa kanda ya video siku mbili baadaye. Katika muda wa siku kadhaa, Boko Haram liligawanyika katika makundi, na mapambano kati ya pande mbili yaliripotiwa mwishoni mwa mwezi huo.
Makundi yalikuwa na tofauti za kiitikadi. Al-Barnawi alidai kwamba wana jihadi ni vyema walenge katika kuwashambulia wakristo na malengo ya kijeshi. Shekau anadai mtu yoyote ambaye anahsindwa kufuata mafundisho ya Allah na mtume Mohammed – ikiwa nipamoja na waislam waiso na msimamo mkali – wanaweza kulengwa katika ghasia. Kundi la tatu, linaloongozwa na Mamman Nur, linakaribiana na imani zaz al-barnawi lakini hawana uhusiano na IS.
Mgawanyiko, kutegemea ungedumu, huenda ungelisaidia jeshi la Nigeria kudhibiti eneo ambao walimelikamata tena, ingawaje ushirika wa jeshi la kikanda unaopambana na Boko Haram umeonyesha mataizo yao wenyewe. Wachambuzi wanasema majeshi nadra sana kushirikiana nje ya mipaka kama walivyotarajia.
Tishio kubwa kwa jeshi huenda likawa ni Civilian JTF. Amnesty International imesema imerekodi manyanyaso yaliyofanywa na kudni, ikiwemo kupigwa na kuuliwa kwa washukiwa wa Boko Haram. Huku vita dhidi ya Boko Haram ikiwezekana vinapungua, maelfu ya vijana wa kiume ambao walishika silaha kutetea jamii zao wanaomba wapatiwe ajira katika jeshi na mashirika ya usalama.
Serikali inajaribu kuwaingiza wapiganaji, kwa kiasi kutokana na maslahi binafsi, amesema Zenn.
“Kuna baadhi ya watu ambao wana wasi wasi kama mzozo huu utafikia mwisho, hivi sasa una makundi ya kijeshi ambayo yenyewe yanaweza kuwa hatari hapo baadaye,” amesema. Dhidi ya kuongezeka kwa hali hii, mamlaka ya Nigeria inaendelea kupata maendeleo ya pole pole dhidi ya Boko Haram. Hivi karibuni, mmoja wa wasichana wa Chibok alipatikana, pamoja na mtoto wa miezi sita. Msichana huyo aligunduliwa na wanajeshi walipokuwa wakiwahoji baadhiya mamia ya watu ambao walitiwa ndani wakati wa msako wa karibuni katika msitu Sambisa.
Uokozi ulifika siku chache baadaye kabla ya wanaharakati wanaodai kurejeshwa kwa wasichana wa Chibok kuadhimisha siku 1,000 tangu kutekwa kwao. Kwa Zenn, ukweli ni kwamba wengi bado hawajapatikana ni dalili kwamba Boko Haram halijakaribia kushindwa kama jeshi linavyosisitiza.
“Kama eneo la Boko Haram limepunguzwa na kuwa si lolote, kama serikali inavyosema, vipi wasichana wote hawa hawajapatika?” amesema. “Ungetarajia kuwa serikali imengewapata baadhi yao.”
Kuwapata wasichana – kama ilivyo kwa Nigeria yenyewe – huenda ikawachukua miaka mingi.
JIFUNZE ZAIDI
Angalia ripoti mbali mbali za mitandao ya habari.
Angalia mfululizo wa “Boko Haram: Ugaidi Wafichuliwa”.
Jifunze jinsi VOA ilivyopata video za Boko Haram.
WATU WANASEMAJE
Hirikiana mawazo yako kuhusu "Boko Haram: Ugaidi Wafichuliwa" #terrorunmasked..
Facebook
Twitter
Imeandikwa na Dan Joseph Imetengenezwa na kutolewa na Tatenda Gumbo na Steven Ferri
Waandishi wa VOA Nigeria na Washington, D.C., wamechangia katika ripoti hii.