Boko Haram: Ugaidi Wafichuliwa
Uharibifu wa Ugaidi
Tulivyoripoti habari hii

Boko Haram

 UGAIDI WAFICHULIWA

Kijana wa kiume anapigwa bakora katika eneo la wazi. Wanaoangalia wanapiga kelele “Allahu Akbar.” Wanamgambo wa Boko Haram wanawapiga raia risasi katika moyo na kichwani, wakipuuza maombi ya kuwa hawana makosa na sala zao.

Ripoti ya hapo chini ina picha ambazo ni za siri za video za Boko Haram ambazo VOA imezipata. Ghasia za kutisha huenda zikawakera baadhi ya watazamaji. Zinaonyesha uhalisia na ukatili wa maisha chini ya utawala wa Boko Haram.

UNYONGAJI

Katika mji wa Kumshe nchini Nigeria, mwanamme ameshutumiwa kwa kufanya biashara ya dawa haramu anasali sekund chache kabla ya kuuwawa na Boko Haram. (Video ya Boko Haram)

Katika kijiji cha kaskazini mashariki mwa Nigeria cha Kumshe, kundi la kigaidi la Boko Hara limetenda ghasia na kupotosha vipengele vya sheria ya kiislamu. Makosa kama kuvaa kama mtindo wa magharibi au kupata elimu ya dunia zinabeba adhabu kali sana. Wanaotuhumiwa wauza dawa haramu — kama vile wanatenda makosa walioonyeshwa katika video hizi — walihukumiwa vipigo na vifo.

Kanda ambazo hazikuhaririwa za Boko Haram wakifanya shughuli zao ndani ya eneo la Nigeria ni nadra sana. Kundi hili linajulikana kwa usiri na kuficha kwa makini sana utambulisho wa wanachama na mahali walipo.

Lakini VOA imepata takriban saa 18 za video ambazo hazijhaririwa ambazo kundi hilo imerekodi matukio ya ukatili wao. Picha, kutoka katika laptop ya Boko Haram ilikamatwa katika uvamizi wa jeshi, inabainisha maafa wanayoyapata wanigeria waliokuwa chini ya Boko Haram.

Angalia kanda yote ya video sehemu ya 1: “Boko Haram: Ugaidi Wafichuliwa.”

Kunyongwa kwa wanaume katika mji wa Kumshe, na matukio mengine yanayonyesha wanachama wa Boko Haram wakishuhudiwa wakiendelea na shughuli zao za kila siku  katika eneo walilojitangazia ukhalifa na hiyo ni moja ya sehemu nne za kanda za video za VOA kuhusu, “Boko Haram: Ugaidi Wafichuliwa.”

Rekodi ambazo hazijhaririwa zimefanya machache au hakuna juhudi zozote za kuficha vitendo vya kikatili vya kundi hilo. kwa ishara zote — muda kwenye kanda hizo, marejeo ya wapiganaji, matukio yaliyoelezewa katika matangazo ya habari yaliyosikika kwa nyuma — rekodi ambazo zilifanywa mwishoni mwa 2014 na 2014, kipindi cha upanuzi wa Boko Haram katika eneo la kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Mji wa Kumshe sehemu ambako mauaji yanafanywa na Boko Haram.

NDANI YA SHAMBULIZI

Mpiganaji wa Boko Haram anatembea katika mji wa Banki huku wanamgambo wakifanya shambulizi kwenye kambi ya jirani ya jeshi. (Video ya Boko Haram)

Katika kipindi chote cha uasi wa miaka saba, Boko Haram wameshambulia malengo ya serikali ya kiraia ili kukamata eneo na kupandikiza khofu kote kaskzini mwa Nigeria. Viongozi waliwaahidi vijana wadogo wapiganaji wataingia kujitoa mhanga, kuwaandikisha na kuwapeleka katika mapambano wakiwa na ujuzi mdogo wa silaha na mafunzo machache. Kundi hilo limewateka maelfu ya wanawake na watoto.

Kanda za video zilirekodiwa na Boko Haram zinaonyesha shambulizi moja  kwenye kambi ya jeshi la Nigeria katika mji wa Banki. Wapiganaji wanakusanyika wakati wa asubuhi, na vingozi wanawatayarisha kuua na wao kuuliwa. Shambulizi linageuka vurugu, baadhi ya wanamgambo wanaomba silaha.

Angalia kanda kamili ya video sehemu ya 2: “Boko Haram: Ugaidi Wafichuliwa.”

Baadaye, wapiganaji wa Boko Haram wanawaua raia katika kijiji cha karibu baada ya kwanza kuwataka watafute chakula na fedha. Ufadhili wa Boko Haram unatokana na utekaji nyara na kudai fidia na wizi, miongoni mwa mambo mengine.

KHOFU

Wavulana watatu wanahojiwa na wanamgambo wa Boko Haram baada ya kijiji chao kutekwa. (Video ya Boko Haram)

Kampeni za ghasia za Boko Haram zimeharibi maisha, kusambaza khofu, kuwakosesha makazi mamilioni na kuharibu utaratibu wa kijamii kote kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Wakati wanamgambo wanapokamata kijiji, mahojiano yanafuatia. Lengo: kupata habari kuhusu utiifu na mahali walipo wapenzi wao ambao wamekimbia.

Lengo la Boko Haram, kama lilivyoelezewa na kiongozi wa muda mrefu, Abubakr Shekau ni kutangaza vita vya kidini, kuiondoa Nigeria katika ushawishi wa magharibi na kuweka taifa lenye sheria kali za kiislamu. Kimsingi, kundi hilo limeonyesha huruma kidogo kwa wanigeria waislamu, kushambulizi misikiti na miji mingi yenye waislamu wengi.

Chanzo: Institute for Economics & Peace: Global Terrorism Index 2015 and 2016

KUUTEKA UISLAMU

Mpiganaji wa Boko Haram anatembea katika mji wa Banki huku wanamgambo wakifanya shambulizi kwenye kambi ya jirani ya jeshi. (Video ya Boko Haram)

Kanda ya video vya Boko Haram inaonyesha viongozi wakihalalisha mauaji na wengine ukatili uliotendwa kulingana na iktikadi potofu za kidini. Katika mahakama ya umma, aliyetumwa anasimama mbele.

Anazungumzia kwa niaba ya Abubakar Shekau, kiongozi wa Boko Haram aliye mafichoni huku wanamgambo wakijitayarisha kuwaua wenzao wawili.

Kosa: Ushoga.

Angalia kanda kamili ya video Sehemu ya 3: “Boko Haram: Ugaidi Wafichuliwa.”

Tafsiri ya ghasia ya Uislamu ya Boko Haram inafuata mafunzo ya muanzilishi wake, Mohammed Yusufu. Yusuf alihubirikwamba elimu ya magharibi ni dhambi. Mivutano kati ya mamlaka ya Nigeria na kundi hilo ilisambaa na kuwa ghasia za mauaji mwaka 2009, wakati polisi walipofanya ukamataji kwa wafuasi wa Yusuf na kumuua Yusuf mtaani.

Shekau anaamini kwamba kushambulia malengo ya raia, kuwateka wasichana wa shule na kuwaua “wasioamini” — waislam na wasio waislamu — kunahalalishwa kwa jina la “Jihad.” Wasomi wa kidini nchini Nigeria wamezikataa kwa kauli nzito itikadi za ghasia za Boko Haram.

KILA MTU AMEONDOKA

Kituo cha petroli ambacho kimeachwa karibu na kambi ya watu wasio na makazi huko Bama, kimeharibiwa na Boko Haram. (VOA)

Harakati za kundi hilo zimewakosesha makazi zaidi ya wa Ngieria milioni mbili na zimepelekea kusambaa kwa ukosefu wa usalama wa chakula.

Hivi leo, miji mingi ambayo awali ilikuwa chini ya udhibiti wa Boko Haram imekombelewa na jeshi la Nigeria na mataifa jirani. VOA News ilisafiri kwenda kaskazini mashariki mwa Nigeria mwezi September 2016 kuthibitisha madai ya jeshi juu ya kuboreka kwa usalama na kujionea wenyewe gharama ya maisha ya binadamu kutokana na uasi wa Boko Haram.

Wakiwa wamefuatana na msafara wa magari 12 yenye vifaa vya kivita, VOA ilitembelea miji ambayo iliwahi kuonekana kuwa si rahisi kufika na kushuhudia jinsi wanigeria wanavyojaribu kuijenga tena. Katika maeneo yasiyo chini ya udhibiti wa jeshi, Boko Haram bado ni tishio. Kundi linaendelea kufanya mashambulizi ya mabomu na mashambulizi ya silaha kwa raia na malengo ya kijeshi.

Chanzo: International Organization for Migration, Nigeria, December 2016

KUMSHE HAIPO TENA

Wanaume wawili kutoka Kumshe wameguswa na picha zinazoonyesha ukatili wa Boko Haram kijijinikwao. (VOA)

Mkimbizi mmoja kutoka Kumshe amethibitisha kwamba kijiji chake kilikuwa ni eneo la kunyongwa watu na kupigwa katika rekodi za video zilizochukuliwa na Boko Haram.

Zinaonyesha za eneo la kijiji zilizochukuliwa kutoka kwenye video, alianza kulia.

Angalia kanda ya video yote sehemu ya 4: “Boko Haram: Ugaidi Wafichuliwa.”

Imeandikwa na Salem Solomon Imetengenezwa na kutolewa na Tatenda Gumbo na Steven Ferri