Waandishi wa habari wa VOA kote ulimwenguni waliangaza maudhui yanayohusu thamani ya mtoto wa kike kuonyesha jinsi gani biharusi mtoto anavyothaminiwa na familia zote mbili : Ile anayoihama na nyingine anapoolewa. Na ni thamani gani anayolipa mtoto huyo wa kike anapoolewa akiwa chini ya miaka 18? Kupata maoni kutoka sehemu mbalimbali duniani wakati tunaripoti, timu za wanahabari VOA – zikiwakilisha lugha 12 – ziliposti picha za video fupi zinazohusu watoto wa kike na wanawake wanaoeleza uzoefu wao kama maharusi na mama ambao bado ni watoto. Picha hizi za video zilizokuwa zimewekwa katika mtandao wa Facebook ziliangaliwa na mamilioni ya watu na maelfu ya maoni kutumwa, kutoka viunganishi vya hisia zinazokuwa katika muundo wa picha (emojis) hadi malumbano ya hoja yakiunga mkono au kukosoa ndoa za utotoni.

Dar Es Salaam, Tanzania

‘Nimewaita maafisa polisi’

Baada ya kukataa kuolewa, msichana huyo mwanafunzi alitafuta msaada kwa wanaharakati wa uwezeshaji wanawake.