
Marekani
Usa
Dyersburg, Tennessee, USA Miaka michache baada ya ndoa, Katie bado hana ushahidi halisia wa ndoa yake na Ben kwa sababu anasema “dada yake aliiba pete yake ya harusi”.
Kwa Umoja wa mataifa na wizara ya mambo ya nje Marekani, Katie ni muathirika wa unyanyasaji wa haki za binadamu. Lakini kile alichokifanya kilikuwa halali kabisa na ni jambo la kawaida katika jimbo la kati magharibi la Missouri, mahala ambako ndoa ilifanyika upande wa pili wa mpaka kutoka Dyersburg huko kaskazini-magharibi ya Tennessee mahala anakoishi Katie.
Zaidi ya watoto 78,000 Marekani wapo au wamekuwa kwenye ndoa, kulingana na ripoti mpya iliyotolewa na Shule ya umaa ya chuo cha UCLA.
Afya (http://newsroom.ucla.edu/releases/child-marriage-in-us-threatens-well-being-ucla-study) Missouri wakati huo ilikuwa mahala mashuhuri kwa ndoa za utotoni kwa sababu jimbo hilo halikuwa na umri maalumu unaoruhusu msichana kuolewa. Watoto wa miaka 14 pekee ndio walihitaji idhini ya jaji. Mwaka 2018 jimbo liliongeza umri halali wa msichana kuolewa kua miaka 16. Tennessee bado hairuhusu msichana kuolewa akiwa na umri wa miaka 16.
Mama wa Katie, Evelyn Montgomery alitia saini leseni ya ndoa kwa sababu tu, Katie alikuwa na ujauzito wa Ben. Kwa kuwa alikuwa chini ya umri wa miaka 18, Ben angeweza kufunguliwa mashtaka ya kubaka mtoto mdogo.
“Nilimweleza mama yangu, nitamlea vipi mtoto huyo, wakati yeye nakiwa gerezani na mimi sina kazi?” Anaeleza.
Kwa Evelyn, ndoa haikuwa suluhisho zuri. “Lakini nilihisi wakati huo, ndio lilikuwa chaguo pekee,” anasema.

“Sijali kile mtu mwingine anachofikiria, nina mpenda Ben.”
Ben Burns, kushoto, alikuwa na miaka 30 wakati alipomuoa Katie, kati kati, aliyekuwa na miaka 16 na mjamzito. Aliozesha Ben ili asipelekwe gerezani kwa mashtaka ya kumbaka mtoto mdogo. Baada ya miaka saba, bado wameendelea kuwepo kwenye ndoa na wanawalea Zena mwenye miaka 6 na mtoto wa Ben wa kiume mwenye miaka 18 kutoka kwenye ndoa nyingine. (Picha na Carolyn Presutti wa VOA)
“Katie anasema “sijali kile mtu yeryote anachofikiriwa. Ninampenda Ben. Ndoa imedumu kwa miaka minane. “Hivi ndivyo ilivyo.”
“Katie anasema “sijali kile mtu yeyote anachofikiriwa. Nina mpenda Ben. Ndoa imedumu kwa miaka minane. “Hivi ndivyo ilivyo.” Katie akifanya mashara anakiri kwamba mume wake ana umri takribani sawa na baba yake. Na anapishana umri wa miaka mitano na mtoto wake wa kiume kutoka ndoa ya awali, ambaye anaishi nao katika nyumba yenye kuta za njano iliyopo kando ya njia ya reli nje ya mji.
Kutoka basi la shule hadi kuolewa From school bus to wedding
Ashley Duncan mwenye umri wa miaka 15 na ulikuwa mwaka wake wa kwanza kwenye shule ya sekondari katika kijiji cha Steele kwenye jimbo la Missouri. Akiwa amekaa kwenye basi la shule shangazi yake aliingia ndani ya gari na kumueleza, teremka kwenye gari Ashley, unaolewa leo hii. Kama Burns, alipokuwa mjamzito.
Lakini hakutaka kuolewa na baba mwenye mtoto wa miaka 18.
Ashley anaeleza, wakati mhubiri alipokuwa akizungumza, na mimi ninatakiwa kusema Ndio ninakubali, mimi nilisema ninafikiri. Sio Ashley wala mume wake aliyefanikiwa kumaliza shule ya sekondari. Waligombana sana na hatimaye walitengana.
Wakati unapokuwa mdogo, una tabia ya kuamini watu pale wanaposema wanakupenda. Na unapenda kusikiliza watu wanapokueleza kitu cha kufanya, anasema Ashley.
Ashley anawapenda watoto wake wawili wa kiume na anawalea watoto hao pamoja na watoto wawili wa kiume kutoka kwa rafiki yake wa kiume ambao wana umri wa miaka 5 na 6. Ametengana na mume wake kwa miaka kadhaa, lakini hawezi kumudu masharti ya talaka hadi akubali kulipa nusu ya gharama. Ashley anatamani kama mtu angemuonya kuhusu madhara au matokeo ya ndoa za utotoni.
Anaelezea kwamba hivi sasa anahisi kama amepoteza muda mwingi wa maisha yake, na hakukuwa na sababu ya hilo kutokea.
**Wasichana wote wamepoteza maisha yao ya utotoni. Katie anasema amekosa kucheza SOFTBALL na kutofahamu kinachoendelea Duniani. Ashley amekosa kukutana na marafiki zake na kuwa nao pamoja usiku kucha.
Anasema baada ya kuolewa, marafiki zake hawakuwa karibu tena na yeye.
Lost Childhoods
Wote Katie na Ashley waliolewa Pemiscot County Courthouse huko Caruthersville kwenye jimbo la Missouri, mji wenye watu chini ya 7,000. Upo katika eneo moja la kusini mwa Missouri linaloitwa Bootheel, kwa sababu ya umbo lake. Bootheel moja ya maeneo maskini sana huko Missouri, inapakana na majimbo matatu na kufanya iwe kituo cha ndoa za utotoni.
Kabla hawajapitisha sharia kali mwaka 2018 ambapo umri wa kuolewa hivi sasa ni miaka 16, jimbo la Missouri halikuwa na masharti kwa mtu mwenye umri wa miaka 15 kuolewa na ilihitajika mtu yeyote mwenye chini ya miaka 14 kupata ruhusa ya jaji ndipo aolewe. Hivi sasa kama mtu mmoja yupo chini ya miaka 18 na mwingine ana miaka 21 au zaidi ya hapo, serikali ya jimbo haitoi leseni kwa wawili hao kuolewa.
Pam Strawbridge anayefanya kazi na kaunti, alitia saini leseni nyingi za ndoa katika taaluma yake ya miaka 40 na alichukia kutia saini leseni alizosema zilikuwa za watoto. Strawbridge anasema sahihi yake ipo kwenye kundi la mtoto mmoja mwenye miaka 13 ambaye alikuja Missouri kuolewa.
Anasema sidhani kama wana uzoefu wa kutosha. Na kwa kweli hawafahamu ndoa inatakiwa kuwa jukumu la milele.
Ending the Cycle
Katie na Ben Burns wana nyumba ambayo imejaa mbwa, paka n ahata nguruwe wachanga. Binti wa wapenzi hawa, Zena hivi sasa yupo darasa la kwanza. Ndoa za utotoni sio miongoni mwa ndoto za Burns kwa binti yake. Katie anasema unatakiwa kusubiri. Hakika unatakiwa kuwa na umri wa miaka 18, kwa mtazamo wangu. Unahitajika kuwa mtu mzima unayejitambua.
Kiwango cha ndoa za utotoni nchini Marekani
2 | 4 | 6 | 8 | 10 |