Tanzania

‘Nimewaita maafisa polisi’

somo moja muhimu sana ambalo Mwanahamisi Abdallah amejifunza kama mwanafunzi nchini Tanzania ilikuwa wakati wa sherehe za mahafali ya shule ya msingi wakati alipokuwa na umri wa miaka 14. Mfanyakazi wa shule aligundua kwa wanafunzi kadhaa walikuwa wameacha shule ili kuolewa, alitoa namba ya simu ya dharura kwa msichana yeyote anayelazimishwa kuingia katika suala la ndoa.

“Niliiandika namba hyo na kwenda nyumbani,” anasema mwanahamisi, ambaye hivi sasa ana miaka 15, ambatokea katika kijiji kimoja karibu na mji wa pwani wa Kilwa katika mkoa wa kusini mashariki mwa nchi wa Lindi. Aliihifadhi namba hiyo.

Siku moja mama yake alimfahamisha kuwa karibuni huenda ataozeshwa, Mwanahamisi anasema alilia sana. “Sitaki kuolewa!” mama yake alipuuza kilio chake, na kumpa moyo alimueleza mwanamme anayetaka kumuoa ni kijana na mtu mzuri.

Bibi yake Mwanahamisi alimpa simu ya mkononi ili aweze kuwasiliana na mumewe mtarajiwa. Badala yake, aliitumia simu kupanga mipango ya kukimbia.

“Haraka, nilipiga simu kwa maafisa polisi. Waliniuiza nipate jina la huyo mwanamme na siku ya ndoa,” Mwanahamisi anakumbuka hilo. Mara alipopata maelezo machache kutoka kwa mama yake na kuyapitisha kwao, polisiwalimjulisha afisa wa eneo. Alifika nyumbani kwao katika siku ya mkesha wa harusi, na kumuulliza msichana kama alikuwa anataka kuolwa. Wakati huo, alikuwa ameshafahamu kuwa mwanamme huyo alikuwa na wake watatu.

“Niliposema hapana, sherehe za harusi zilisimamishwa,: amemueleza afisa.

Afisa ustawi jamii wa wilaya hatimaye alipanga msichana huyo ahaie kwenye makazi maalum mjini Dar es Salaa, kiasi cha kilometa 325 (maili 200) kutoka kaskazini.

Picha ya Mwanahamisi Abdallah, katikati, amekaa kwenye ngazi pamoja na wasichana wengine wanne.

Mwanahamisi Abdallah, katikati, na wasichana wengine walio katika mazingira hatari. Msichana huyo mwenye umri wa miaka 15 alifanya kazi na washauri baada ya kukimbia ndoa ya utotoni. (Picha Na Faraja Filbert Dogeje wa VOA News)

Ndoa za utotoni barani Afrika chini ya jangwa la Sahara

Mwanahamisi alikimbia ndoa ambayo hakuitaka, kinume na wasichana wengine wadogo huko barani AFrika chini ya jangwa la Sahara. Eneo hilo duniani lina viwango vikubwa vya ndhoa za utotoni, huku zaidi ya wasichana milioni 3 kila mwaka wakiolewa kabla ya kufikia umri wa miaka 18, kwa mujibu wa Idara ya Umoja wa Mataifa ya Kuhudumia Watoto. Maelezo yapo UNICEF notes katika ripoti ya 2019.

Wasichana wanasukumwa katika ndoa za mapema kwasababu ya mila au ukosefu wa njia mbadala, utafiti umebaini hivyo. Watoto wengi walio katika hatari ya ndoa za mapema huwa wanatokea katika nyumba maskini katika maeneo ya vijijini na wana fursa chache za kupata elimu rasmi. Barani Afrika chini ya jangwa la Sahara, wasichana 7 kati ya 10 wanamaliza elimu ya msingi, lakini ni 4 tu kati ya 10 wanamaliza elimu ya ekondari, kwa mujibu wa Benki ya Dunia. Ripoti ya (Novemba 2018). (https://www.worldbank.org/en/news/press-release/2018/11/20/Africa-loses-billions-of-dollars-due-to-child-marriage-says-new-world-bank-report), taasisi hiyo imesema wanawake wenye elimu ya sekondari, “wako katika nafasi nzuri ya kufanya kazi, na wanalipwa mara mbili zaidi kuliko wale ambao hawana elimu.”

Benki ya Dunia inakadiria kwamba ndoa za utotoni huenda zikagharimu jumla ya $bilioni 63 ikiwa ni mapato ambayo yamepotea katika muda wa maisha ya wanawake katika dazeni ya nchi za Afrika ambazo zinawakilisha nusu ya idadi ya watukatika bara hilo. Viwango vya ndoa za utotoni kawaida ni vikubwa sana huko Afrika Magharibi na Kati, huku wasichana 4 kati ya 10 wanaolewa wakiwa na umri mdogo UNICEF inasema. Viwango vya Niger viko juu mno, ni wasichana 3 kati ya 4 (76%).

“Kuna taratibu nyingi (kijamii) ambazo zinazisukuma familia kutaka watoto wao wa kike waolewe mapema,” anasema Moustapha Ibrahi,, meneja mipango katika taasisi maendeleo na masuala ya kibinadamu ](https://plan-international.org/organisation). Hasa katika tamaduni na mila kwa watu maskini, familia zinafurahi zawadi kutoka kwa bwana harusi mtarajiwa, kama vile fedha taslimu au mifugo, na khfu ya kuaibishwa kutokana na mimba za nje ya ndoa, anasema. Thamani ya msichana inakuja kwa kuwa mtunza nyumba na kupata watoto.

“Familia kubwa zinaonekana ni zenye nguvu. Familia kubwa zinaonekana kuwa ni mali,” Ibrahim anaongezea, ingawaje anasema kuwa dhana inabadilika, hasa katika maeneo ya mijini.

Kampeni ya Umoja wa Afrika kumaliza ndoa za utotoni](http://au.int/en/sa/cecm), ilianza mwaka 2014, “imezungumziwa sana barani humo,” anasema Mundia Situmbeko, afisa wa mawasiliano kwa ushirika wa Afrika kwa ushirika wa ulimwengu Wasichana siyo Maharusi.

Kampeni imelenga nchi 30 zenye kiwango cha juu, ikiwemo Niger na Tanzania, na kuelezea mafanikio binafsi na ya kijamii katika kuchelewesha ndoa. Inataka “[kuunga mkono hatua za kisheria na kisera]](https://www.globalpartnership.org/blog/enough-silence-early-marriage-and-girls-lack-access-school)” tkulidna hakiza binadamu, kuongeza uwelevu wa umma na kujenga harakati za kijamii. Situmbeko anasema, AU imeonyesha heshima kwa viongozi wa kijadi na kidini, nakupaaza sauti zao katika mikusanyiko.

“Waondiyo wanaoweza kuisukuma mbele ajenga ya mabadiliko ya kijamii na thamani inayowekwa kwa mtoto wa kike,” anasema.

Nchini Tanzania, ambako Mwanahamisi aliiacha familia yake ili kukwepo kuolewa, kiasi cha theluthi moja ya wasichana wanaolewa wafikapo umri wa miaka 18 kwa mujibu kuwa Wasichana siyo Maharusi. Hatimaye, zaidi ya robo moja ya wasichana wote wanamaliza elimu ya sekondari. Katika tripoti ya Januari kuhusu Tanzania, Benki ya Dunia ilifanya hesabu zake kwambakumaliza ndogo za utotoni na kujifungua ukiwa naumri katika nchi kunaweza kufanya akiba ya nchi kufikia mpaka dola bilioni 5 kwa mwaka ifikapo 2030, kwa kupunguza kasi ya ukuaji wa idadi ya watu na kupunguza mahitaji kwa huduma za kijamii na kuminya miundo mbinu.

Serikali ya Tanzania na mahakama zilikuwa na changamoto ya kisheria kuhusu ndoa za utotoni. changamoto ya kisheria limepeleka mahakama kuu kufuta vipengele viwilikatika sheria ya ndoa nchini mwaka 2016, na kimsingi kuongeza umri wa chini kwa wasichana kuolewa uwe miaka 18 kutoka miaka 15. Lakini serikali ilikataa rufaa dhidi ya maamuzi hayo mwaka jana katika misingi kwamba umri mdogo wa chini kwa hakika unawalinda wasichana kutopata mimba nje ya ndoa. Mamuzi yalitolewa hivi karibuni. Wakati huo huo, serikali inawafukuza shule wasichana wanaopata uja uzito.

Picha ya Mwanahamisi Abdallah akitumia cherehani.

“Ndoto yangu ni kuwa mwanamitindo wa juu!”

Mwanahamisi Abdallah, 15, anachukua mafunzo wa kupika na samaa ya nguo pamoja na masomo ya kompyuta na masuala ya fedha.

Licha ya sheria hiyo, wasichana wa kitanzania kama Mwanahamisi wameweza kupata msaada wakati wakikabiliwa na ndoa ambao hawazitaki.

Kama Mwanahamisi, wanaweza kulifuata jeshi la polisi Tanzania, ambalo limetoa mafunzo kwa timu mbali mbali kote nchini kujibu malalamiko yanayohusumanyanyaso ya majumbani au ngono, usafirishaji haramu wa binadamu au vitisho vya watto. Mamlaka zinaweza kuwaondoa watoto kutoka katika hali ambayo wanaamini si salama.

Mwanahamisi alifika Dar es Salaam na kuishi katika nyumba inayoendeshwa na Kiota cha afya na maendeleo ya wanawake (KIWOHEDE), shirika ilisilo la kiserikali abapo pia linaendesha vituo vya muda kwa ajili ya wasichana na wanawake walio katika mazingira hatarishi. Amefanya kazi na washauri ili kuondokana na kiwewe na amesonga mbele kwa kujiunga na masomo ya kompyuta na uhasibu, kupika na sanaa na utengenezaji vitambaa.

“Ndoto yangu ni kuwa mwana mitindo mkubwa sana!” anasema.

Zamani alikuwa mtu wa aibu na mwenye kukubali, hivi sasa amekuwa kichoche,” anasema Justa K. Mwaituka, mkurugenzi mtendaji wa KIWOHEDE. Anasema Mwanahamisi alikuwa ni muhimu katika kuanzisha kundi la vijana wa rika ambalo hukutana kila siku kuimarisha malengo ya elimu, uwezeshaji wanawake, na kuwa na sauti kubwa kusema lini ni muafaka kuolewa.

Mawasiliano na familia ya Mwanahamisi ni muhimu. Mama yake msichana anatuma salaam kupitia mwafanykazi wa ustawi wa jamii, ingawaje Mwanahamisi hana mawasiliano ya moja kwa moja, mpaka pale afisa ustawi wa jamii na KIWOHEDE watakapoamua kuwa yuko tayari, na hali ni salama.

Lengo ni kuwa na mawasiliano na familia lakini wanachelewesha kukutana, anasema Regina Mandia, ambaye anasimamia nyumba ambayo Mwanahamisi anaishi.

“Kuharakisha watoto hawa kuolewa ni kukatiza ndoto zao.”

Mtizamo wa Kimataifa

Asilimia ya wanawake wanaoolewa chini ya umri wa miaka 18
10% 20% 30% 40% 50% 60%
Ramani

Marekani

6.2

Namba ya watoto walioolewa kwa kila watoto elfu moja, wenye umri kati ya miaka 15-17

(That's about .6%
of 15- to 17-year-olds .)

The term ‘child marriage’ is used to refer to both formal marriages and informal unions in which a girl or boy lives with a partner as if married before the age of 18. An informal union is one in which a couple live together for some time, intending to have a lasting relationship, but do not have a formal civil or religious ceremony. The main sources of such data are national censuses and national household surveys, predominantly the Multiple Indicator Cluster Surveys (MICS) and Demographic and Health Surveys (DHS).

In 2003, UNICEF and partners agreed to focus on five indicators:

  • Percentage of women 20 to 49 first married or in union by age 15 and 18, by age group
  • Percentage of girls 15 to 19 years of age currently married or in union
  • Spousal age difference
  • Percentage of women currently in a polygynous union, by age groups
  • Percentage of ever-married women who were directly involved in the choice of their first husband or partner.