Mrama Wahamiaji Waafrika Ugenini

A group of 104 sub-Saharan Africans on board a rubber dinghy wait to be rescued 25 miles off the Libyan coast. (Reuters)

Imeripotiwa na Abdulaziz Osman na Nicolas Pinault
Imehaririwa na Peter Cobus

Februari 2016

Utangulizi

Wakati Ulaya inaendelea kupokea mmiminiko wa wahamiaji kwa idadi kubwa sana, hadithi za wale wanaokimbia vita nchini Syria, Iraq na Afghanistan zimetawala vichwa cha habari.

Lakini hadithi za waafrika wa chini ya jangwa la Sahara, wahamiaji wa uchumki na wakimbizi kuhusu  ukosefu sugu wa uthabiti  na ghasia za  kikanda , si sana kuwafikia wengine ulimwenguni  — mpaka pale safari zao  zinapokabiliwa na majanga.

Kati ya takriban waafrika 130,000 ambao wamejaribu kusafiri mwaka 2015 peke yake, wengi wao walikuwa wanakimbia majanga ya kila siku na umaskini uliokithiri — kile ambacho wengine wanakiita ni athari za mabaki ya enzi ya ukoloni.

Katika kambi za muda mjini Rome, mhamiaji raia wa Gambia, Morro Saneh mwenye umri wa miaka 16 anaelezea kwa ufupi: “Sisi tunataka kuishi kama binadamu.”

Wakitokea mbali zaidi hadi Sahel, njia mbili kuu kwa wahamiaji wa chini ya jangwa la Sahara  kufika katika “ardhi ya matumaini” zinapitia Libya, ukosefu  wa sheria kutokana na vita na mapigano kati ya taasisi za serikali Ni hapa, katika kiini cha baada ya mapinduzi ya kiarabu, ambako mapambano mbaya yalimuondoa  dhalimu Moammar Gadhafi madaraka na kuonekana kuwa ni kweli linaweza kutokea: “Mediterranean itakuwa ni bahari ya vurugu.”

Wakiwa wanakabiliana na maji, katika  eneo kubwa la bahari wakiliacha jangwa nyuma, walikabiliwa na uamuzi mzito wa safari yao: ama wajiingize katika hatari ya kuvuka mawimbi mazito, ambayo yamechukua maisha ya  wahamiaji  3,771  mwaka 2015,  katika siku ambayo ni tulivu ni dhahiri watafika katika fukwe za kusini mwa Italy. Lakini pia kwa wale ambao wana bahati kufika kwenye pwani ya mapumziko, pepo haraka inageuka na kuwa aina fulani ya ahera kwenda kutubu dhambi. Kama walivyo wenzao wa Mashariki ya Kati, mara nyingine wasafiri wasio na utaifa  wanajikuta wamekwama kati ya wafanya magendo ambao wanatumia hali yao ngumu bila ya kuogopa, na serikali ambazo haziwapi ruhusa ya kubaki. Hizi ndiyo hadithi zao.

Sehemu ya Kwanza: Njia

Sehemu ya Kwanza: Njia Barabara ya kuingia Ndani

Wahamiaji wa Kiafrika wanaanza safari yao hatari kutoka Niger kuelekea mwambao wa Libya. (Reuters)]

Kwa mujibu wa Taasisi ya Kimataifa ya Uhamiaji, kiasi cha asilimia 90 ya wahamiaji wa kiafrika wanawasili Ulaya wakipitia Libya; takriban asilimia 10 wanapitia Misri. Raia wa Afrika Magharibi  — wengi wao kutoka Senegal, Gambia, Ghana na Nigeria   — wanawasili Sabha, Libya kupitia Mali na Niger kabla ya kufanya safari yao kwenda Tripoli, mara nyingine wanasafiri maili 10,000 katika muda wa wiki mbili, na mara nyingine inawachukua miaka.

Kutoka Pemba ya Afrika, wasafiri wengi raia wa Eritrea na Somalia wanawasili kupitia Ethiopia, Kenya, Uganda na Sudan.

Video ya simu ya mkononi  wahamiaji wakivuka bahari ya Mediterranean kwa boti ya wasafirishaji kutoka Misri. (VOA/Abdulaziz Osman)

“Kusafiri kupitia Sahara ni mbaya sana kuliko kusafiri kwa njia ya bahari. Baharini ama utakufa au utanusurika,  lakini hautakumbwa na madhila na maumivu yasiyokwisha.”

– Hafsa, mwanamke wa kisomali, mjini Rome

Njia zote hukutana nchini Libya, ambapo ukanda wa pwani ni kiasi cha maili 160 za nyutiko hadi Lampedusa, moja ya visiwa vikubwa vya Pelagie nchini Italy, ambacho ni karibu sana na ardhi ya Ulaya.

Video ya simu ya mkononi ya wahamiaji wa Kisomali katika meli ya Umoja wa Ulaya. (VOA/Abdulaziz Osman)

Eneo la jangwa la Sahara linawakilisha chini ya asilimia 15 ya mafuriko ya watu wasio na makazi barani Ulaya mwaka 2015, ikiwa ni idadi kubwa sana bara hilo kuwahi kuona tangu Vita vya II vya Dunia. Karibu wote wanaowasili wanatokea Italy. Kinyume na jirani yake Ugiriki, ambayo imeona ongezeko kubwa la uhamiaji ambalo limechochewa na vita nchini Iraq, Syria na Afghanistan, mmiminiko wa Italy kutoka eneo la Sahara  bado umekuwa na idadi ile ile  kama ilivyokuwa miaka iliyopita.

“hakujakuwa na “ongezeko: la uhamiaji nchini Italy mwaka huu,” anasema Frederico Soda, mkurugenzi wa IOM wa ofisi ya uratibu kwa Mediterranean ambayo ina makao yake mjini Rome.  Kwa mfululizo, idadi ziko sawa na zile za 2014, lakini  mgawanyo wa kikabila na kikanda uko tofauti — ni kwa vile, raia wachache wa Syria, ambao hivi sasa wanatumia njia za Balkan. Ni zaidi kwa wa Afrika Magharibi, ambao kimsingi ni wahamiaji wa uchumi, na pengine hawaangaliwi kwa kiasi kikubwa. Na hivyo sivyo kwa wale ambao wanakimbia hali ngumu ya ukosefu wa uthabiti na ukosefu wa usalama huko Pembe ya Afrika.”

Mahojiano na Federico Soda, Mkurugenzi wa IOM, Ofisi ya Mediterranean, Rome, Italia (VOA/Nicolas Pinault)

Sehemu ya Pili: Libya

Sehemu ya Pili: Libya Kando ya Dimbwi: Kuelekea Libya

Malapa yaliyoachwa na mhamiaji katika jangwa karibu na mpaka wa Libya. (Reuters)

Kwa wahamiaji wanaosafiri, Libya ni kitendawili. Kituo chao kikuu mara kwa mara kinakuwa na njia ambazo ni hatari katika jangwa la Sahara, pia ni msingi wa kujiingiza katika safari hatari kuvuka Mediterranea kwa kutumia mashu. Kwa mujibu wa takriban wasafiri wote ambao wamehojiwa, ni kipande hatari cha safari yao na  mategemeo yao kupata bahati njema.  Ni hifadhi ya makundi ya kihalifu na taasisi za kigaidi, katika taifa la Afrika Kaskazini ambalo limeshindikana  — ambalo liliwahi kuwa ni kituo kikuu cha ajira kwa wananchi wa kusini mwa jangwa la Sahara —limekuwa ni eneo la vitisho.  ripoti ya karibuni ya  United Nations kwa kina imeelezea mateso, utumwa, ubakaji na kurubuniwa na magenge ya kihuni, wafanya magendo na maafisa wa serikali ambao wanasimamia jela za Wizara ya Mambo ya Ndani.

“walibya katika eneo la mpakani wanatupiga kwa mabomba ya plastiki, wanatulazimisha kusukuma magari yaliyojazwa mchanga…. wanatupanga mstari kwenye jua kali sana huku wao wakila na kunywa mbele yetu.”

– Husein Muhidiin, mwanamme wa kisomali, mjini Milan

Licha ya kuwepo kwa maelezo ya kina kuhusu ukiukaji mkubwa, wahamiaji wengi hawafahamu hatari, anasema Soda wa Taasisi ya Kimataifa kwa Uhamiaji: “Hawafahamu kwamba wafanya magendo wanazidi kuwa wakatili.”

Kama Sama Tounkara mwenye umri wa miaka 23 kutoka Mali anavyoelezea, “Mjini Tripoli, kila siku inatulazimu tukimbie.”

Mwanamke wa Nigeria akiwa amekwama kwenye bandari ya Tripoli, Tripoli, Libya (AP)

Mhamiaji kutoka Mali, Sama Tounkara anazungumza kuhusu maisha Libya. (VOA/Nicolas Pinault)

Sehemu ya Tatu: Ushuhuda

Sehemu ya Tatu: Ushuhuda Kivuko: Ushahidi

Mhamiaji kutoka Somalia, Rahma Abukar Ali na mwanawe Sofia wakiwa Gelsenkirchen, North Rhine-Westphalia, Ujerumani (VOA/Abdulaziz Osman)

Mama mwenye umri wa miaka 33 ana watoto saba,  amejifungua katika manowari ya kijerumani Schleswig-Holstein; raia wawili wa Ethiopia wenye umri wa miaka 16 wamezuiliwa na wafanya magendo mpaka familia yao ilipe fidia ya $8,000 kwa kila mmoja wao; raia wa Somalia  amewaona wanaume wakinywa mkojo wao wakati kifo kikiwasogelea huko jangwani. Kila mmoja ana hadithi ya kushangaza, lakini hatima yao inategemea kuvuka Meditteranean.

Ushuhuda wa video: Rahma Abukar Ali, 33, Somalia: Wakati Rahma Abukar Ali alipopanda meli ya wahamiaji nchini Libya hapo Agosti 22, alijua kuwa safari yake itakuwa ni mwanzo wa kitu kipya na matumaini au itakuwa ni mwisho wa maisha yake.

Ali alitumia miezi mitano ya mwisho ya mimba yake  akiwa njiani kutoka Somalia kwenda kwenye pwani ya Libya, akisafiri  maili baada ya maili kupita kwenye jangwa la Sahara lenye joto kali. Ahueni yake ya kutembea: ni pale alipolala au alipokuwa kajibana kwenye magari yaliyokuwa yamejaa watu huku wengine wakikimbia eneo la Pembe ya Afrika lililokumbwa na vita.

“Nilikuwa nasikia kizunguzungu;nilikuwa nimechoka sana kwasababu ya safari ndefu,” anasema. Akiwa amepani kujifungua sehemu yoyote ile lakini si Libya, alipanda meli chakavu licha ya hatari.

“Nilikuwa tayari kufariki na mtoto wangu ambay hajazaliwa au nifanikiwa kufika Ulaya,” amesema.

Bada ya kujifungua kwenye manowari ya Ujerumani katikati ya Mediterranean yeye na mtoto wake wa kike, Sophia, walianza kuelekea kwenye kituo cha wakimbizi karibu na Dusseldorf. Anasubiri majibu ya maombi yake ya hifadhi.

Libya huenda ikawa somalia ya……..Mediterranean. Utaona maharamia huko Sicily, huko Crete, huko Lampedusa. Utaona mamilioni ya wahamiaji  haramu. Vitisho vitakuwa mlango wa pili.”

– Saif Gadhafi, ambaye aliwahi kuwa mrithi wa Kanali Moammar Gadhafi, akizungumza na vyombo vya habari , Machi 7, 2011.

Mahojiano na mhamiaji wa kisomali Rahma Abukar Ali, mama wa mtoto Sofia wakiwa Gelsenkirchen, North Rhine-Westphalia, Ujerumani  (VOA/Abdulaziz Osman)

Ushuhuda wa video: Sama Tounkara, 23, Mali: Katika kambi ya muda inayoendeshwa Chama cha Msalaba Mwekundu mjini Rome, Sama Tounkara  anajaribu kupumzika kidogo kabla ya kuendelea na safari yake upande wa kaskazini.

Kukimbia vita sugu nchini Mali na ukosefu wa ajira mwaka 2014, kijana mrefu wa Bamako alisafiri hadi Gao kabla ya kuvuka mpaka wa Algeria na kuingia Tamanrasset. Baada ya miezi sita ya kufanya kazi za ujenzi huko Ghardaia, alikwenda Libya na kugundua kuwa mambo yanazidi kuwa mabaya.

“Mjini Tripoli, kila siku watu huwa wanafika na silaha na kuchukua fedha zetu,” anakumbuka hilo. “Au watatuambia tuwafuate tukafanya kazi ndogo ndogo, lakini, ukweli ni kwamba walituibia.”

Usiku mmoja wanaume waliovalia sare walifika na kumwambia asaidie kusfisha  kuzunguka kambi, alitishiwa tena kwa bunduki. Kosa lake? Kutaka alipwe kwa kazi aliyofanya. Hiyo ikamfanya aamue kukimbia. Kuvuka Mediterranean kwa kutumia boti ndogo iliyojaa takriban wahamiaji 146, alidhani kuwa huenda akafariki. Lakini baada ya takriban saa saba akiwa baharini, aliokolewa na melki ya Ulaya.

Mahojiano na mhamiaji Sama Tounkara  (VOA/Nicolas Pinault)

Ushuhuda wa video: Dalmar and Ahmed, both 16, Ethiopia: Baada ya kiasi cha mwezi mmoja nchini Italy, vijana hawa walio na umri mdogo bado wanakhofia kutaja majina yao ya kweli.

Wote ni wanafunzi wa zamani, walishawishiwa kuondoka nyumbani na marafiki zao ambao tayari walikuwa wameanza maisha mapya Ulaya.

“Kuna sababu nyingi kwanini tulindoka,” anasema Ahmed. “Kuna ukosefu wa ajira, na hata wale ambao wamehitimu kabla ya sisi walikuwa hawana cha kufanya wamekaa bure mitaani, kwahiyo tuliamua kuondoka.”

Bada ya Addis Ababa wafanya magendo waliwaendesha hadi sehemu ambako watatembea kwa miguu kwa takriban saa nane kutoka kwenye mpaka wa Sudan, walijiunga na wahamiaji wengine na kujitayarisha kwa safari ya kuvuka Sahara. Baada ya siku tano za kutembea na kuomba msaada wa usafiri katika magari yaliyojaa watu, hatimaye waliwasili Adjabiya, mji mkuu wa Wilaya ya Al Wahat kaskazini mashariki mwa Libya, kiasi cha kilometa 150 kusini mwa Benghazi.

“Katika siku ya tano ya kusafiri jangwani, tuliishiwa na maji,” Ahmed anakumbuka. Walikabidhiwa kwa wafanya magendo wengine ambao ni katili zaidi, ambao mara kwa mara waliwatesa wahamiaji ambao walikataa kuzishinikiza familia zao kulipa fidia kwa njia ya simu.

Makovu aliyonayo Dalmar ni ushahidi kwa wiki sita alizokaa kwa wafanya magendo wa Libya.

Mhamiaji kijana wa miaka 16 akielezea safari yake kutoka Ethiopia mpaka Milan, Italia (VOA/Abdulaziz Osman)

Ushuhuda wa video: Morro Saneh, 16, Gambia: Katika kambi ndogo ya muda ya wahamiaji mjini Rome, Morro Saneh anakumbuka usiku ambao aliondoka nyumbani. Ilikuwa ni mkesha wa mwaka mpya 2015 na, akikhofia kushindwa kwa jaribio la mapinduzi dhidi ya Rais Yayah Jammeh, kijana huko aliondoka bila ya kuieleza familia yake kuhusu mipango yake. Baada ya kufika Kaolack, Senegal, alilipa $3,000 ili kuweza kufika Bamako, Malim, ambako alikaa kwa takriban mwezi mzima akiuza maji mitaani. Huko Algadez, Niger, alikuwa mtengeneza matofali; mjini Tripoli, polisi walichukua fedha kidogo alizokuwa nazo na kumsweka jela kwa siku 33..

Akiwa na azma ya kufika Sweden, Saneh hata hivyo anawaonya vijana wa kiafrika ambao wanatafuta maisha huko Ulaya: “Kama ikimlazimu kufanya tena, kamwe asingefanya hivyo. Hatari ni nyingi.”

Mahojiano na mhamiaji kutoka Gambia Morro Saneh (VOA/Nicolas Pinault)

Sehemu ya IV: Walanguzi

Sehemu ya IV: Walanguzi 'Magafe' Mkosa Huruma

Wavushaji haramu walichoma mkono wa mhamiaji huyu wakati wa safari hatari kutoka Pembe ya Afrika kwenda Libya  (Obtained by VOA/Nicolas Pinault)

Kila mwaka, safari za wahamiaji na wakimbizi zinazalisha mabillioni ya dolla, na magenge makubwa ya uhalifu ya kimataifa yanaongeza ujanja wa kupata faida. Wakijua kuwa wahamiaji wana matumaini ya maisha mazuri, uongozi wao kupita katika njia zisizo za kawaida kwenda Ulaya ni muhimu sawa na zilivyo za kinyonyaji.

Kuanzia Khartoum mpaka Calais, hadithi za mateso zinafanana mno: walanguzi wanatesa wahamiaji katika jangwa, wakizima sigara katika mikono, uso au kifua cha wahamiaji, wakiwafunga pamoja kama wanyama na kuwajaza ndani ya magari yanayosafiri katika jangwa la Sahara, na mara nyingine hata kuwafunga ili watoe malipo mara tu wafikapo Libya.

Mhamiaji kutoka Eritrea anazungumza kuhusu safari yake ya kutisha kupitia Libya, hadi Milani, Italia. (VOA/Nicolas Pinault)

 ” Mara nyingine Magafe hakuweza kutupa nguo au mkaa kupika chakula…Niliona wapishi wetu wakitumia baadhi ya viatu vyetu na makoti kupikia ili tusife njaa.”

– Hafsa, mwanamke wa kisomali,  mjini  Rome akitumia maneno maarufu ya kisomalia kuwatambua wasafirishaji

Mahojiano na mhamiaji kutoka Sudan Abdallah Arku. (VOA/Nicolas Pinault)

Hata Italia, walanguzi wanafanya kazi zao wazi wazi. Raia mmoja wa Eritrea aliambia VOA alionywa asijisajili serikalini, huku wengine wakishikiliwa katika nyumba moja Catania kwa zaidi ya siku 10, na kuachiliwa tu pale walipochangisha na kulipa maelfu ya dolla.

Mhamiaji mwenye miaka 16 kutoka Ethiopia aliyeshikiliwa na wavushaji haramu, Milan, Italia. (VOA/Abdulaziz Osman)

Wale ambao wana uwezo wa kuendelea na safari wanatafuta mtandao wa waongozaji wasio halali ambao mazingira yao ya kazi yanabadilika: kuanzia raia wenzao ambazo wanavusha katika bahari ya Mediterranean hadi Waalbania kutoka makundi Mafia ambao wanashirikiana na kambi za kupokea wakimbizi kaskazini ya Ufaransa. Hata wahamiaji wasio na fedha wanaweza kuendelea na safari kuelekea kaskazini wakihakikisha kuwa watafanya kazi kulipa madeni yao. Kulingana na Giovanni Abbate wa shirika ya IOM, kwa wasichana, hiyo inaweza kuwa kuingizwa katika umalaya.

Giovanni Abbate, mwanasheria na afisa wa IOM, Sicily, Italia. (VOA/Nicolas Pinault)

Sehemu ya Tano: Hitimisho

Sehemu ya Tano: Hitimisho Njia iliyo mbele: Maisha hatarini, Sera yenye utata

Eneo la mabanda la wahamiaji linaloitwa ‘The Jungle’ ni nyumbani kwa maelfu ya watu wenye matumaini ya kuvuka kuanza maisha mapya Uingereza. (VOA/Nicolas Pinault)

Khofu iliyotanda daima ni uanamgambo wa al Shaba ambao umemsukuma Nimco Muse Ahmed, mama maskini wa kisomalia mwenye watoto wawili, kusonga mbele kupitia katika jangwa kubwa duniani, eneo moja la vita  na kuvuka bahari kwa kutumia usafiri boti usio na uhakika.

Ilikuwa ni baada ya kiwasili Vienna, inayotambulika kihisia “Mji wa Ndoto” ambao uko juu katika  Uko katika orodha ya UN kuwa una ufanisi, alipojitupa kutoka kwenye ghorofa ya juu ya iliyokuwa kambi ya jeshi hadi kwenye sakafu.

“Niliwekwa katika hali ya kutokuwa na fahamu kimatibabu kwa muda, nilivunjika miguu yote  na uti wa mgongo,” anasema  Ahmed, anaelezea hali iliyofuata ya kupata nafuu baada ya jaribio lake la kwanza la kujiua  huko Austria  katika kambi ya wakimbizi iliyopo Traiskirchen, achuo cha zamani cha kijeshi kilichopo nje kidogo ya mji mkuu.

Khofu iligeuka na kuwa hali ya kukata tamaa katika kipindi cha majira ya vuli, muda mfupi baada ya kufahamu kuwa ombi lake la kuomba hifadhi limekataliwa. Akijaribu kujipa moyo wa kulipuuza  ilikuwa ni kikwazo kingine kwenye njia ya kuelekea katika maisha bora, anasema hilo liliamshwa na kupigana kati ya wakimbizi wa kisomali na wa Syria juu ya kupotea kwa simu ya mkononi, ndiyo lilimsukuma ukingoni.

“Nilikuwa nimekata tamaa kwasababu ya matatizo na ukweli ni kwamba bado nilikuwa sijakubaliwa kama muomba hifadhi,” anasema wakati huo aliruhusu khofu imfanye akate tamaa. “Watu barani Afrika — hasa Somalia  — nignependa kuwaeleza, ‘hakuna kitu barani Ulaya, kwahiyo wasiwe na ndoto na hilo.’”

‘Nauona ukweli hivi sasa. Theluji. Sijawahi kusikia njaa nilipokuwa Afrika hivi sasa nipo hapa naisikia njaa.’

– Nimco Muse Ahmed, mkimbizi wa kisomali nchini  Austria

Mahojiano na mhamiaji wa Kisomali Nimco Muse Ahmed (VOA/Abdulaziz Osman)

Mambo yote yanafanana yanayowakumba wahamiaji wengi kutoka  jangwa la Sahara ambayo yale wanayapitia  baada ya kuwasili Ulaya, mambo muhimu ya habari za Ahmed hata hivyo yanabainisha  magumu yanayowakumba wengi ambao wamebanduliwa kutoka kwenye makazi yao .

Kama walivyo wengi katika takriba wakimbizi wengine milioni 1 ambao wamewasili mwaka 2015 pekee, akiwa anasaka maisha bora ikimaanisha kuiacha familia yake nyuma — ambaye akiba yake yote iliishia katika safari ya baharini na kubahatisha kunusirika kifo — halafu akajikuta  hana nyumba, na bila ya hati ya kusafiria, hana utaifa, kwenye bara la kaskazini ambalo halijui.

Kinyume na raia wa Syria, Afghanista na Iraq ambao ni idadi kubwa ya wale wanaowasili barani Ulaya, hata hivyo, Ahmed anasema jangwa la Sahara linakabiliwa na aina fulani ya ubaguzi usio wa kawaida. Kote katika vituo vya uhamiaji na kwenye kambi kote barani humo, anasema, wanatendewa kama raia wa daraja la pili na wenzao wa kiarabu na wa Afghanistan. Ugomvi kuhusu simu ya mkononi ulimsukuma yeye kushindwa kujizuia, anaelezea kwasababu ilikuwa moja ya mfululizo wa malumbano madogo  mdogo miongoni mwa jamii za raia wa kigeni, na hilo lilitarajiwa kumalizika kama ilivyomalizika mengine. Kwasababu wakimbizi wa Afghanistan wameelimika wanaweza kuelezea habari zao kwa maafisa wa kambi, wenzake wa Afrika wanaokaa chumba kimoja, bila ya kujali iwapo waliiba simu, huenda hatimaye wakabeba lawama.

Vituo vikuu vinavyolengwa wa wahamiaji kutoka kusini mwa jangwa la Sahara

Ramani inayotokana na Tume ya Ulaya ikionyesha vituo vya wahamiaji kupitia Italia, ambavyo hutumiwa na wahamiaji kutoka kusini mwa jangwa la Sahara kuwasili Ulaya.

Sera katika Utata

Kwa wakimbizi kama Ahmed, hakuna majibu rahisi. Huku mataifa wanachama 28 wa EU yakijitahidi kukabiliana na mmimiko usio tegemewa wa wahamiaji mwaka 2015, kushugulikia  deni la Ugiriki na mashambulizi kadhaa ya kigaidi, umoja wa kisiasa uliohitajika kubuni suluhisho haujapatikana. Kwa hakika, utabiri   wa karibuni  wa hali ya kiuchumi barani Ulaya  unaashiria  ongezeko la wahamiaji milioni 3 katika mwaka unaofuata, na Uingereza, moja ya mataifa “matatu makubwa” ya Ulaya , inatarajiwa kuitisha  kura ya maoni iwapo iondoke au ibakie katika umoja huo, hatua hiyo huenda ikapelekea migogoro zaidi kuzuka barani humo .

Seng’enge inayozungumza bandari ya Calais jirani na ‘The Jungle’ huko Calais, Ufaransa. (VOA/Nicolas Pinault)

Seng’enge inayozungumza bandari ya Calais jirani na ‘The Jungle’ huko Calais, Ufaransa. (VOA/Nicolas Pinault)

Watunga sera wa Ulaya hawana jibu rahisi la kusuluhisha mzoz; licha ya ahadi ya kuwahamisha waomba hifadhi halali 160,000 kote katika mataifa wanachama, hadi Dec. 12 ni watu 159 tu ndiyo wamepatiwa makazi. Canada imepokea ndege iliyobeba kundi la kwanza la wakimbizi 25,000 raia wa Syria hapo Desemba 11, wakati wabunge wa Marekani wanajiweka tayari kwa duru ya pili ya majadiliano juu ya pendekezo la Rais Barack Obama kuhusu mpango wake wa kupatia hifadhi raia wa Syria 10,000. Uhamiaji ni suala ambalo bado lina mgawanyiko kwa wamarekani katika kampeni, wakati mgombea mtarajiwa wa chama cha Republican Donald Trump ameapa kuzuia  kuingia kwa waislamu  na kuwafukuza raia wa Syria ambao wamewasili kufuatia program ya Obama. Licha ya juhusi kubwa za White House kuhusu sera ya uhamiaji, hata juhudi za kuwapatia visa waliokuwa wafasiri wa  Afghanistan na Iraq katika uwanja wa mapambano.

Kambi ya ‘The Jungle’ huko Calais, France (VOA/Nicolas Pinault)

Kambi ya ‘The Jungle’ huko Calais, France (VOA/Nicolas Pinault)

Kama mataifa binafsi ya Ulaya wanaofanya kazi kupitia maombi ya waomba hifadhi, kusimamia wakimbizi wanaowasili katika maeneo wanayoingia kwa wingi nchini Italy na Ugiriki kwa kiasi kikubwa imekuwa  yameingia katika hali isiyoeleweka  ya kimataifa ya misaada, wanaojitolea na mamlaka za manispaa .

“Kwanini ikiwa ni miezi mingi tangu mzozo, bado ni kama vile wanaojitolea ndiyo wanaotoa misaada kwa wale wanaowasili kwenye fukwe za Ulaya … wakipatiwa msaada wa kuokoa maisha?” Peter N. Bouckaert, Mkurugenzi wa masual aya dharura katika Human Rights Watch, ameandika baada ya kurudi kutoka Ugiriki. “Kwanini wanaojitolea bado wanatoa misaada ya kuokoa maisha ya huduma za afya ambazo si nzuri huko Lesbos, na bila ya magari ya wagonjwa ambayo yametolewa na serikali yoyote au taasisi za kiserikali zilizopo?”

Baadhi ya  ripoti zinakubaliana na ukosoaji huo, zikisema ni vigumu kuwaona wawakilihi wa EU kwenye mstari wa mbele wa mzozo.

“Usimamizi wa mipakani kimsingi ni jukumu la serikali, “ msemaji wa Tume ya Ulaya alisema kupitia barua pepe. “Idara za Tume na Umoja wa Ulaya zinasaidia nchi wanachama na maafisa wa serikali kusimamia hali hiyo – lakini hazichukui nafasi ya nchi wanachama.”

Polisi wakifanya doria karibu na bandari ya Calais karibu na kambi ya ‘The Jungle’ huko Calais, France (VOA/Nicolas Pinault)

Polisi wakifanya doria karibu na bandari ya Calais karibu na kambi ya ‘The Jungle’ huko Calais, France (VOA/Nicolas Pinault)

Mbali ya sera za ndani, EU imeomba kushughulikia kiini cha sababu za watu kukimbia kutoka Afrika. Katika mkutano wa Novemba kuhusu uhamiaji, viongozi wa EU na Afrika walifungua mfuko wa dharura wa dola bilioni $1.9 kwa ajili ya kuzisaidia nchi za Afrika kuwarejesha makwao raia waliokoseshwa makazi. Malta, kisiwa hicho kilikuwa mwenyeji wa mkutano na kituo cha juu kwa  wahamiaji, iliahidi $270,000.

Mwezi mmoja baadaye, maafisa wa EU walizindua mpango wa   $2 billion initiative kumaliza uhamiaji haramu  kutoka Afrika kwa kuchochea nafasi za ajira na program za maendeleo katika bara hilo kwenye mataifa ambayo yanatoa  idadi kubwa ya wahamiaji na wakimbizi.

Mikakati mikubwa ya kuleta uthabiti katika eneo la Mediterranean baada ya kuanguka kwa utawala wa Gadafi. Mwaka 2011, Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Italy, Franco Frattini ametaka kuwepo kwa utaratibu mpya wa kieneo.

‘Kuna mamilioni ya watu weusi ambao huenda wakaja eneo la Mediterranean kuvuka kwenda Ufaransa na Italia, na Libya ina jukumu katika usalama wa Mediterranean.’

– Moammar Gaddafi akizungumza  kwenye  kituo cha  televisheni cha  France 24 television  Machi, 2011.

“EU, mataifa mengine yenye nguvu duniani na taasisi za kimataifa kama vile Benki ya Dunia na Shirika la Kimataifa la Fedha ni vyema haraka waendeleze  mpango wa uthabiti wa  kiuchumi  wa Marshall Plan for Mediterranean  2011 Financial Times op-ed, akielezea juhudi za Marekani kuijenga tena Ulaya Magharibi baada ya Vita vya II vya dunia. “Mpango huu ni vyema uhamasishe taasisi muhimu kwa rasimali mpya za kifedha za Ulaya na kimataifa, katika utoaji wa mabilioni ya dola, kubadiisha chumi za kieneo na kuboresha uwekezaji.”

Frattini amewasili maafisa wa EU kuondoa vikwazo vya biashara kati ya nchi za Mediterranea na kufanya juu ya mkakati pamoja na Marekani, “ambaye bado ina jukumu muhimu .” Ameshawishi fursa zaidi kwa elimu ya juu — kuimarisha nguvu kazi na kuwazuia vijana kuandikishwa katika taasisi za kigaid — na kutaka kuwepo kwa program ya mafunzo ya kazi kote katika eneo zima la Mediterranean, “njia bora ya kuzuia uhamiaji haramu na usafirishaji wa binadamu.”

Kinyume chake, mchambuzi mmoja maarufu wa masuala ya uhamiaji anasema tatizo haliwezi kusuluhishwa kwa kuzungumzia vigezo vinavyoisukuma Afrika peke yake.

“Mzozo wa kweli huko Ulaya ni kushindwa kufanya vizuri kwa Ulaya kubuni jibu la pamoja,” Hein de Haas, mwanasosholojia katika chuo kikuu cha Amsterdamm, ameliambia  The Huffington Post. Huku wakimbizi kutoka kwenye mizozo na wapinzani wa kisiasa wakilindwa na maazimio ya Umoja wa Mataifa, EU kuongeza uwazi wa kiuchumi, amesema, kunafungua njia kwa mahitaji ya wahamiaji kwa vibarua nafuu ambavyo haviendani na masharti makali ya uhamiaji .

“Watu wanazidi kubaini kwamba miaka 25 ya ngomeya Ulaya imeshindwa kabisa,: amesema. “Watu wanawasili, na matokeo makuu imekuwa ni kuongezeka kwa magendo, matatizo kwa wahamiaji na idadi kuwa ya vifo vya mpakani.”

Mahema ya wahamiaji katika ‘The Jungle,’ Calais, France (VOA/Nicolas Pinault)

Mahema ya wahamiaji katika ‘The Jungle,’ Calais, France (VOA/Nicolas Pinault)

Kwasababu mikakati mikubwa ya maendeleo inahitaji maelezo ya ratiba za vizazi — na kwasababu huenda kuna matatizo ya msingi ya mawasiliano kati ya matarajio yaliyopo ya uhamiaji na sera ya biashara na uhamiaji ya Ulaya — Elizabeth Collett, mkurugenzi wa Migration Policy Institute yenye makao yake Brussels, amependekeza kuangalia hilo kwa kiwango kidogo, kikanda  wakilenga mipango ya uchumi.

“Sera ya maendeleo ya kiwango kikubwa peke yake haitazuia uhamiaji,” amesema. “Lakini kuna mambo ambayo ni ya msingi kabisa katika kipindi kifupi ambavyo si muhimu kuhusu kuzuia usafiri, lakini ni kuhusu kujaribu kufungua fursa za kazi ambazo hazihitaji watu kufanya safari za hatari sana kwa kile ambacho kinaweza kuonekana kuwa kikawa na mwisho mbaya.”

Pengine swali ni iwapo EU inaweza kulenga tena juhudi zake katika kile ambacho Gadhafi wa Libya aliwahi kuwapatia: nafasi ndogo ndogo za kibiashara katika ukuaji na fursa za ajira ambapo watu kama vile Nimco Muse Ahmed kwa kiasi inahusu ama kurejea katika maisha ambayo aliyafahamu, wala siyo mapambano ambayo ya kuwa na maisha mapya huko Ulaya.

Hakuna kurejea nyuma

Lakini pia katika juhudi za kuleta uthabiti wa muda mfupi huenda ikawa hakuna maana katika Libya iliyotikisika baada ya enzi ya Gadhafi, ambapo mipaka yake imekuwa haina ulinzi mkali na hivyo kuchochea chuko dhidi ya wahamiaji ambao wanapita kwenda katika mataifa mbali mbali wanachama wa EU. Wakati watunga sera za uhamiaji wanabuni  masuluhisho, huenda  jibu likawepo  siyo katika ofisi za shirikisho huko Brussels, lakini pale ambapo kila hadithi ya ukosefu wa makazi inapoanzia. Kwa makini — au mara nyingi kwa tahadhari kubwa – kupima hatari na mafanikio ambayo yatatoa muongozo kwa wengi wanaotumia njia hii hatari.

Peter Cobus amechangia kuripoti kutoka Washington, DC.

Credits

Imeripotiwa na Abdulaziz Osman na Nicolas Pinault.

Imehaririwa na Peter Cobus.

Sanifu ya Tovuti na Stephen Mekosh pamoja na Dino Beslagic.

Msimamizi mradi Steven Ferri.

Uzalishaji makala na Teffera G. Teffera na Ezra Fessahaye.

Maoni