Dustin Andrews mwenye umri wa miaka 25 alifika kwenye duka la casey, linalouza bidhaa za vyakula na pia kuna kituo cha kujaza mafuta karibu na eneo la kuingia Donnellson, alikwenda kununua biskuti na vitafunio vingine.
“Naishi kiasi cha kilometa 8 kutoka hapa hivyo ni rahisi kuja hapa na kununua vitu vichache,” amesema.
Donnellson, kama ilivyo katika miji mingi midogo katika ukanda wa kilimo, kuna maduka machache katika miji yao na giza linapoingiza au nyakati wa mwishoni mwa wiki hakuna kinachofunguliwa. Duka la vitafunio lililopo kwenye ukingo wa mji ni la kipekee. Miji midogo ya vijijini ambayo iliwahi kushamiri kibiashara kutoka kwa wakulima na wengine waliohusika katika kilimo, lakini kuna wakulima wachache hivi sasa na uboreshaji barabara unawaruhusu watu kusafiri mbali zaidi kwenda kwenye maduka makubwa, kama vile Walmart, ambalo linatoa huduma ya bidhaa mbali mbali na bei zake ni nzuri.
Andrews anafanya kazi katika kiwanda cha siemens huko fort Madison, lakini anaishi mbali ya mji kwasababu anakupenda huko anakoishi.
“Naweza kuacha kile ambacho nakifanya na kuingia katika kilimo kama ningeweza,” ametueleza.
Alipohitimu kutoka shule ya sekondari, alikabiliana na hali ambayo ni ya kawaida mno kwa vijana ambao wamekulia mashambani. Kuna ardhi kiasi na operesheni zake zinatumia zaidi mashine, na hivyo mahitaji ya wafanyakazi ni ya chini mno.
Kazi za kutengeneza bidhaa
Kiwanda cha siemens, ambacho kinatengeneza tani mbili za viwembe kwa ajili ya majenereta makubwa yaliyopo huko iowa na maeneo mengine ya vijijini katika ya Marekani, inaajiri kiasi cha watu 700, wanalipwa zaidi ya dola 20 kwa saa. Andrews alianza kazi huko mara tu baada ya kumaliza masomo ya sekondari, lakini hajawahi kabisa kuacha kuwa mkulima, kufanya kazi bila ya kulipwa kumsaidia mpwa wake ambaye ni mkulima, na kukodisha ardhi karibu na fort Madison, ambako ana ng’ombe 20 aina ya angus na Hereford, pamoja na ng’ombe dume moja kwa uzalishaji.
“Nawakuza kuanzia wakiwa ndama na kuwakuza mpaka wawe na takriban paundi 800 na kuwauza, na kuwaweka baadhi, “ amesema. “Nimejifunza kuhusu kuzalisha ng’ombe kutoka kwa babu yangu upande wa baba, ambaye alikuwa na ng’ombe aina ya angus.”
Yeye na vijana wengi wengine ambao wana mawazo ya kilimo wamezidisha utashi wao. Hali ya uchumi haiko upande wao, huku bei za ardhi zikiwa kubwa na mambo yote yanayohusu kilimo cha kisasa yakiwa ni ya gharama pia. Sensa yam waka 2012 ya wizara ya kilimo ya marekani inaonyesha kwamba mmiliki mkuu wa shamba nchini marekani ni mwanamme mtu mzima mwenye umri wa miaka 58. Kati yam waka 1997 na 2012 kulikuwa na kushuka kwa takriban asilimia 20 katika idadi ya wakulima wapya. Sense imeonyesha kwamba idadi ya mashamba imepungua kwa zaidi ya asilimia nne wakati ukubwa wa shamba la kawaida umeongezeka kwa asilimia 3.8.
Sababu kuu ya Andrews kuwepo Donnellson siku hiyo tuliyokutana ilikuwa kuchukua darasa, ambalo inatakiwa na serikali kwa mtu yoyote ambaye anasafirisha silaha ambayo haiko katika mfuko wake maalum. Katika maeneo mingi ya mijini watu wamechukua madarasa hayo ili kupata kibali cha kubeba bastola, lakini Andrews anasema hana haja na hilo. Yeye ni mwindaji ambaye anataka urahisi wa kuweza kubeba bunduki kubwa kwenye gari lake tayari kwa kuitumia wakati wa msimu wa uwindaji. Anawinda swala, bata na bata bukini.
Jambo moja Andrews na vijana wengi kama yeye katika eneo hilo hawalifurahi ni siasa. Alistahili kupiga kura kwa miaka saba na huenda angeweza kupiga kura mwaka 2012 na katika uchaguzi wa rais mwaka 2016, lakini alijiweka kando katika uchaguzi nyakati zote hizo mbili. Amesema hakuna masuala ambayo yanamtia wasi wasi.
“Nina matumaini kuwa upepo wa biashara ya nishati unaendelea kuvuma,” amesema, “trump si shabiki mkubwa wa hilo.”
Andrews, ambaye kazi yake ni kukagua mashine za kutengeneza viwembe kama zina hitilafu na halafu kuzikarababi, binafsi ananufaika na upepo huo katika kiwanda hicho cha nishati, lakini ana machache ya kusema kuhusu manufaa ya kimazingira watu wengi wanajihusisha na nishati mbadala.
Iowa ni moja ya majimbo yenye nishati ya upepo katika taifa hili, wakizalisha theluthi moja ya umeme unaendeshwa na mashine za upepo. Lakini ingawaje anakhofia kuwa utawala wa trump unasisitiza kuhusu maendeleo ya nishati ya kiasili huenda ikaathiri kiwanda chake na pengine kazi yake, Andrews haonekani kufikiria kuna mengi anayoweza kufanya kuhusu hilo.