Kwenye barabara moja ya kijijini yenye ghala za kuhifadhi chakula na mashine ya umwagiliaji wakati wa jua la majira ya baridi kali, tunamuona mwanamme mmoja akifanya kazi katika gereji ya wazi.
“Natengeneza vyuma vichakavu hivi sasa,’ mwanamme huyo mwenye umri wa miaka 57 anaelezea. “ nadhani inayaweka mawazo yangu na mikono yangu itumike vyema.” Anajipatia fedha kidogo kwa kuuza vyuma ambavyo vimevunjika kutoka kwenye vifaa, anasema, lakini si vingi.
Mpaka miaka miwili iliyopita, alikuwa mfugaji ng’ombe, akiwa na ng’ombe 24 kwa ajili maziwa. Lakini kama ilivyo katika maeneo mengi madogo ya ufugaji, mambo hayakuwa mazuri, na ikawa vigumu kuhimili ushindani wa mashamba makubwa.
Anasema sheria ya huduma nafuu ya afya – mpango wa bima ya afya maarufu kama Obamacare – umefanya mambo kuwa mabaya zaidi, na kumlazimisha yeye na marafiki zake wengi kutumia fedha nyingi zaidi kuliko wanavyomudu, kwa bidhaa ambayo hawaitaki.
Miongo kadhaa kwa kile wanachokiona kuwa sera kali za serikali zimechochea ghadhabu na mashaka kwamba program kama hizi zinaweza kuboresha maisha ya wamarekani, mwanamme huyo anasema akionyesha ghadhabu yake wazi wazi. Kama ilivyo kwa dazeni ya watu katika kaunti nyingine ambazo zimempigia kura raia trump baada ya awali kumuunga mkono rais Obama, anasema wakazi wa trempealau hawaamini tena wanasiasa wa asili.
“Fedha zote zinakwenda mijini,” anasema. “watu wote wa maeneo ya vijijini mara hii wamesema, tumetosheka.”
Kumpigia kura trump, kwake yeye, ilikuwa kwa kiasi kikubwa ni kura dhidi ya Obamacare.
Hata hivyo anakiri, “imefanya kazi kwake.”
Miaka miwili iliyopita, alifanyiwa upasuaji wa dharura kwa maambukizo kwenye mguu wake, hali ambayo ilimuathiri vibaya sana na kumlazimu kuacha kazi. Pato kuu hivi sasa ni hundi ya wasio na ajira kutoka serikalini.
“Nilikuwa na Obamacare kwa takriban wiki mbili kabla ya kunifanyia upasuaji,” anasema.
Mkulima wa zamani ni miongoni mwa zaidi ya watu 200,000 ambao awali walikuwa hawana bima hapa katika jimbo la winsconsin, ambako hivi sasa wana bima ya afya na zaidi ya watu milioni 2 ambao, kwa hivi sasa, wana mafao ya ziada, kwa mujibu wa takwimu za serikali.
Bado anasema karibu kila mtu anafahamu hakuugua tangu asaini bima ambayo wametakiwa kufanya hivyo na serikali na wengi wameathiriwa na gharama zinazojitokeza.
Hata kama angekuwa anaitaka, anasema ingekuwa vyema iwe ni uamuzi wake, na siyo uamuzi wa serikali.
Akiwa ana chechema kidogo, na mwenye wasi wasi wa kuchunguzwa amekataa kutaja jina lake, ametueleza tuwasikilize wakazi wengine ambao wanasema walimuunga mkono trump kwa sababu mbali ya kuichukia sheria ya huduma ya gharama nafuu za afya.
“Nafaka hazina thamani yoyote. Nguruwe hawana thamani,” anasema na kuelezea jinsi bei za vyakula zilivyopanda, na eneo lake linavyoathiriwa. “ na hivi sasa wanatutaka tununue bima ya afya?”