Ripoti Maalum ya VOA

Nje ya Barabara Kuu

Sauti za wananchi kutoka miji midogo na vijijini, Marekani

Pamoja na migogoro inayoendelea Washington, urais wa Donald Trump bado unaendelea kupewa ushirikiano mkubwa na kambi ya chama chake, hususan katika maeneo ambayo wapo wamarekani weupe, vijijini Marekani. Hawa ni “wanaume na wanawake waliosahauliwa” ambao Trump aliwaahidi mengi, watu ambao wanahisi kuwa serikali zilizopita zilikuwa zimejikita katika kile kilichokuwa kikidaiwa kama upendeleo kwa wasomi wa mijini na pwani. Waandishi wa VOA hivi karibuni walisafiri katika maeneo ya wilaya  za vijijini kando kando ya Mto Mississippi ambazo zilibadilika kutoka rangi “blu” kwenda rangi “nyekundu” – ambazo zilikuwa zikimuunga mkono  mdemokrat Barack Obama, na baadaye kumuunga mkono mrepublican Donald Trump mwaka 2016.  Walizungumza na wakulima na maseremala, wafanyakazi wa viwandani na wastaafu katika maeneo haya yenye wazungu wengi, wakristo, jamii za wafanyakazi na watu wa tabaka la kati, wale ambao walikuwa na matarajio makubwa ya mabadiliko, na wale waliokuwa wamechoshwa na hayo. Hizi hapa ni simulizi zao.